Baadhi ya Lecturers wa Mzumbe wana degree Feki - VC wao naye FEKI

Toeni data ili serikali iweze kupata ukweli na kuchukua hatua kwani wengi walio serikalini wanaiangalia JF na wengine watafikishiwa.Lengo ni kuisafisha nchi kila kona,sekta hizi za elimu ni muhimu ziangaliwe ili kuzuia ufisadi wa elimu itakayozaa wasomi mafisadi.
 
Kamisheni ya vyuo vikuu chini ya Professor Mayunga wamewafuta udaktari wahadhiri saba wa Mzumbe university wiki iliyopita pamoja na aliyekuwa VC wa Mzumbe university Bwana warioba kwa kuwa na shahada za uongo.
Imebaki kwa mawaziri wenye PhD feki kuchukuliwa hatua kama Nchimbi na Kamala na wenzao.
 
Mhhhhhhh hapa wasomi mmekabana makoo. Mimi nilimaliza darasa la nne hivyo uko kwenu siko. Sijui chuo kipi bora kuliko kingine. Lakini nijuavyo mwamba ngozi siku zote uvutia kwake.
Nilipokuwa na soma darasa langu la nne niliona shule yangu ikiwa juu sana. Nyakati zile tukiziita middle school. Hata imefikia wengine eti wanalinganisha darasa la nne la enzi yangu na kidato cha nne cha shule ya kata. Sijui ni kweli? haya na hiyo jadilini nyie wasomi wa MU na UDSM. Hawa wengine wa Tumaini na Saut wao wako kimya wanaangalia mvutano wa ubora wenu.
Nadhani wao kwa kuwa hawasemwi hapa ni bora kuliko nyie MU na UDSM.
 
Inashangaza kusikia eti Ikulu haina habari kuwa kuna mawaziri katika serikali ya Muungwana wenye degree feki!! Hawa jamaa; Mtawa, salva mnaishi dunia gani?Mnatakiwa muwe current ili mumpe briefing muungwana ajue kuwa ana mawaziri YEBO YEBO!!
 
Inashangaza kusikia eti Ikulu haina habari kuwa kuna mawaziri katika serikali ya Muungwana wenye degree feki!! Hawa jamaa; Mtawa, salva mnaishi dunia gani?Mnatakiwa muwe current ili mumpe briefing muungwana ajue kuwa ana mawaziri YEBO YEBO!!

YEBO YEBO?? sio member wa humu JF kweli??
 
YEBO YEBO?? sio member wa humu JF kweli??
Hahaha,

Mkuu Waberoya, huyu hakulenga Yebo Yebo ambaye ni member wa JF.

Alimaanisha kusema "Mawaziri mbumbumbu" au tuseme "Mawaziri 'hamnazo'".

Najua ulitaka kuamsha mjadala...
 
hili ni suala muhimu saana.hatuwezi kupata magraduate walio wazuri kwa kutumia malecturer ambao hawana viwango vya elimu vinavyostahili. C hili tu bali kuna watu sawa wana phd lakini c za fani anayofundisha,matokeo yake wachache wa chini wanbebeshwa mzigo pasipo sabau za msingi Hakuna haja ya kuwaajiri watu wenye PHD zisizoweza kuzaa matunda nchini. Bora waajiriwe wachache watakaofanya kazi kwa ufasaha. Kwani hizi PHD Wanalipwa hela nyingi pasipo kufanya kazi yoyote, naomba hili lichunguzwe kwenye vyuo vya ufundi hapa nchini,huko ndo worse zaidi.
 
Nadhani baada ya kuondoka "DR" wa kujipa warioba kwa sasa Mzumbe imejipanga na ipo safi kwa upande wa waalimu.

Nikiwa kama muanzisha mada karibu miaka mitatu iliyopita nimeona ni jukumu langu kusema NIMESHUKURU KWA KILIO CHETU KUSIKILIZWA.

Nitakuja baadaye na Mzumbe Dar campus....

Stay tuned

Hivi NUNGWI yupo wapi jamani?
 
asante kiongozi kwa muongozo..very good thinking
 
Dr Chijoroga ambaye ni Mentor wa CEO wa shirika la Nyumba alifeli MBA YA Ubelgiji.
 
.......hivi yule kihiyo alishatakiwa kwa sheria ipi? maana wengine wengi wanapeta tu. au mambo yapo tofauti? Maana hii ni hatarii kwa Taiifa letu>
 
hivi vyuo 1.PWU 2.Commonwealth Open University sidhani kama vipo recognised internationally!
 
huyo DR, ASSAD MUSSA si mkweli anachuki binafsi na mzumbe kwani hapo UDSM kwenye kitengo chake yupo Baisi ambaye alikwenda marekani akarudi na phd feki na hadi sasa yupo pale. wapo wengi udsm
naleta data soon.

Tunazisubiri hizo data lakini kwa angalizo tu Baisi sio Dr. na wala hajawahi kujitambulisha popote hivyo.

Tiba
 
.......hivi yule kihiyo alishatakiwa kwa sheria ipi? maana wengine wengi wanapeta tu. au mambo yapo tofauti? Maana hii ni hatarii kwa Taiifa letu>
Hii iko tofauti acheni ushabiki, Kihiyo alidanganya kuwa ana cheti ambacho hajawahi kukisomea wakati hawa wana Phd ila tu vyuo walivyosomea sio acredited hapa kwetu. Huko baadae vinaweza vikawa assessed na Phd zao zikaonekana safi. Wala haina maana kuwa hawa hawana uwezo wa kupata Phd, uwezo wanao kutokana na pass zao za undergraduate kama wakijiunga na chuo chochote nina uhakika watapata Phd bila wasiwasi.
 
Mzumbe kumzawadia PhD Waziri nchimbi wiki hii mnaweza kusoma gazeti La Mwananchi la leo. najiuliza kwanini Diploma,Masters na PhD zote Bwana Nchimbi amesomea Mzumbe tu? nilitegemea kwa vile kituo chake cha kazi za Waziri Nchimbi ni Dar vizuri angefanya PhD yake University of Dar-Es-Salaam.Mzumbe bado kuna mashaka hata kama Warioba kaondoka.
 

Kama kweli wew ni wa Mzumbe taifa limekula hasara kubwa mno, yani sisi walipa kodi tunakusomesha ila ajabu ni kwamba hata kanuni za uandishi bora huzijui, haiwezekana uandike makala yenye mvuto wa kusoma hivi ila hata space umeshindwa kuweka, Kweli mtoa mada alichokisema kuwa kuna wafundishaji ni kweli kabisa kwa sababu wangekuwa wazima wasingeweza kutoa mtu kama wewe na kumpa shahada, yani hata sisi ambao hatujasoma tunakushangaa sana!!!

Jitahidi mkuu uhudhurie hata semina fupi ya uandishi ili angalau na wewe uonekane angalau una elimu kidogo hata kama ni ya Mzumbe!!
 
Mkuu taarifa kama hizi huwa nazipenda sana but vp kuhusu source????? hebu tupatie angalau source ili na siss tuwe current zaidi!!
 
... Wakati WALIOKWENDA SHULE wakiendelea na tujimambo twao twa spacing na fulustopu, wenzetu MLIOELIMIKA msijisahau mkachotwa na kimjadala, badala yake endeleeni kutumia ELIMU (sio vyeti) kutatua matatizo yetu, na kutumia rasilimali lukuki kututoa hapa shimoni tulipo. Waacheni wenye vyeti walumbane kuhusu rangi za vyeti vyao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…