A
Anonymous
Guest
Ndani ya Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) kuna majengo yanayotumiwa na baadhi ya wizara. Majengo haya ni hosteli za Chuo kutaja Wizara chache zilizopo mpaka sasa ni Kilimo, Viwanda, Maendeleo ya Jamii, Afya, Mifugo na Uvuvi.
Ili kufika katika majengo hayo unapita hosteli za wanafunzi zinazopakana na Wizara hizo.
Utaudhika na harufu kali ya choo, inaonekana vyoo vimejaa na maji machafu hayajatolewa kwa muda mrefu. Harufu ni kali sana.
Hapa wanapita viongozi wa Serikali na Watumishi wa Umma wengi kwenda na kurudi nyumbani. Harufu hii inawapata vizuri tu.
Wanafunzi wapo hapo kila siku harufu wanaishi nayo bila shaka.
Sasa mvua zinanyesha na huenda harufu hii inatokana na kutoboka kwa mabomba au kuharibika kwa mifumo ya maji machafu.
Magonjwa ya kuambukiza yakilipuka nani wa kulaumiwa?
Nani mwenye wajibu wa kutoa taarifa kwamba Vyoo ninanuka ?
Wanafunzi, walinzi au waoita njia?
Tunaomba Uongozi wa UDOM uchukue HATUA haraka kudhibiti harufu hii.