Baadhi ya mambo ambayo hupelekea kudorora kwa kampuni

Baadhi ya mambo ambayo hupelekea kudorora kwa kampuni

Jc Simba

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
300
Reaction score
423
Katika mambo ambayo yanaonyesha kwamba kampuni ina matatizo ya kifedha ni pamoja na kutokua na taratibu maalumu za utendaji wake hasa katika matumizi ya fedha.

Tatizo hili huwa sio la kushtukiza bali huchukua muda mrefu likiwa linaonekana hapa utasikia wafanyakazi wakilaumu labda mkurugenzi ametumia fedha vibaya au kuna mambo yamefanyika kwa kutumia fedha pasipo kuelewana vizuri baina ya uongozi.

Wakati mwingine hata mishahara huanza kuchelewa kulipwa lakini huwa hakuna sababu ya msingi ambayo huwekwa bayana zaidi ya blabla za hapa na pale tu.

Hivi vyote huchangia kushusha morali ya utendaji kazi kwenye kampuni husika na kupunguza ushirikiano kati ya wafanyakazi na uongozi.

Mara nyingi morali ikishuka husababisha hata mambo yasiende kama yanavyotakiwa yaani huchangia kuharibu zaidi kwa kuwa na utendaji mbovu na huku ikiwaacha wafanyakazi wakifikiria kuhusu hatima yao.

Hapo wengine hufikiria kuacha na wengine kuelekeza nguvu zao kwenye mambo mengine na hivyo kuzidi kuharibu mustakabali ya kampuni husika.

Pia kuna suala la kushuka kwa mapato kwenye kampuni husika hapo kutokana na kuwa na sintofahamu ya wafanyakazi kuhusu hatima yao basi utakuta hata uzalishaji unapungua na kusababisha kushuka kwa mapato.

Pia hutokea kucheleweshwa kwa malipo ya wafanyakazi na sitahiki nyingine.yaani kama incriment zilikua zinatolewa mwezi wa saba utashangaa mara zimeanza kutolewa mwezi wa kumi na kitu au hata sizitolewe iwe danadana tu kana kwamba hamna la maana linaloendelea.

Hili hata kwenye maisha ya kawaida tu utakuta mambo haya yanaanza nafikiri sio tu kwa kampuni hata taasisi nyingine na hata serikali kuna mambo ya aina hii hutokea. Muendelezo wa haya masuala ya danadana husababisha taharuki kubwa kwa watu wote wasijue uelekeo wanaouendea.

Kuajiriwa na kuacha kazi kwa wafanyakazi mara kwa mara .Yaani unakuta watu wameajiriwa baada ya muda mfupi wameacha kazi kutokana na sabau hizo tajwa eidha hkuna ongezeko la mishahara kama inavyoonekana kwenye mkataba au kelele za kejeli za muajiri au dharau za muajiri kama muhindi koko.

Kwa hiyo kampuni inakosa sifa ya kuwa na wafanyakazi wa k udumu maana kila mara wanaondoka kutafuta maslahi mazuri zaidi wenyewe wanaita Green Pasture.

Hapa utaona wanaajiriwa baada ya muda wanaondoka kwa mfumo wa namna hii tegemea kuwa na utendaji mbovu maana watabaki wale ambao sio competent kwenye soko na hivyo kampuni itaendelea kuwa hovyo kila uchao.

Malalamiko ya wafanyakazi hayashughulikiwi kwa wakati. Hii utakuta kwa mfano wafanyakazi wanadai malimbikizo ya likizo,madaraja,nyongeza za mishahara yao lakini utakuta hayafanyiwi kazi kwa wakati unaotakiwa hii husababisha wafanyakazi kuacha kufanyakazi bila morali kuua jina la kampuni yaani kampuni inakosa sifa maana sifa za kampuni huenezwa na wafanyakazi hata kama hawaisifii ili kwa jinsi watakavyokua wanaishi itawaonyesha wengine waelewe tu kwamba kuna hali nzuri kwenye kampuni yao.
 
Ila pia tukae tukijua siyo kila siku mambo yanakuwa mazuri...

Kuna mwaka kampuni zinaingiza faida sana mambo yanakuwa smooth, kuna mwaka mambo yanakuwa siyo mazuri kuchelewa kupo...

We should stay positive always...

Cc: mahondaw
 
Daahh kama hii kampuni yetu mwezi wa 3 hatujalipwa mishahara afu ajabu hata nssf hawaweki mbali na hapo hawatupi notisi yoyote kuhusu kuchelewa kwa mishahara!Yaani wanaona tuna shida ya kazi sana tena ni cheap lebour.

Nafkiria hatua y kuchukua ili nilipwe hizo stahiki nipite hivi.Sasa sijui hata naanzia wapi?Nisaidieni wenye uelewa zaidi
 
Daahh kama hii kampuni yetu mwezi wa 3 hatujalipwa mishahara afu ajabu hata nssf hawaweki mbali na hapo hawatupi notisi yoyote kuhusu kuchelewa kwa mishahara!Yaani wanaona tuna shida ya kazi sana tena ni cheap lebour.

Nafkiria hatua y kuchukua ili nilipwe hizo stahiki nipite hivi.Sasa sijui hata naanzia wapi?Nisaidieni wenye uelewa zaidi
Poleni sana hapo mishahara ikichelewa mpaka tar 15 ya mwezi mwingine inaweza fungua kesi mahakamani
 
Huyu jamaa nahisi anauzoefu sana katka mambo haya, kapiga mulemule au umeeajiriwa na Mhindi JC SIMBA
 
Back
Top Bottom