Baadhi ya mambo usiyoyajua kuhusu Baraka Shamte

Baadhi ya mambo usiyoyajua kuhusu Baraka Shamte

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
BARAKA SHAMTE...
Lugha ya Kiingereza inakuwa kila siku kwa kuja na maneno ambayo mimi sikupata kuyajua hapa zamani.

Siku hizi kuna neno ''trend.'' ambalo nadhani lina maana, ''lililopo sasa.''

Habari inayo-''trend,'' mitandanoni hivi sasa ni Baraka Shamte.

Baraka Shamte haitaji kuelezwa si kwa sura wala kuwa yeye ni nani?

Baraka Shamte kwa muda niliomfahamu ni mtu hodari wa kuzungumza Mashaallah.

Hili nalijua kwa kumsikia kwa masikio yangu katika vyombo vya habari na pia kwa kuwa na mahojiano na yeye ya uso kwa macho nyumbani kwake Mkunazini.

Mahojiano haya yanaweza kuwa kwangu mimi ni ''Classic,'' samahani ikiwa mtaona najipigia zumari langu mwenyewe.

In Shaa Allah nitaeleza habari hii baadae.

Namkumbuka Baraka Shamte mwaka wa 1995 Malindi, Zanzibar wakati wa Uchaguzi Mkuu akipita barabarani huku akinadi kwa Kiingereza kilichonyooka akisema, ''We have won the election we are going to form the government.''

Anatembea barabara ya Malindi kavaa unifomu za CCM anatangaza ''ushindi,'' wa Komando Salmin Amour dhidi ya Maalim Seif.

Nilikuwa Zanzibar kufuatilia uchaguzi ule ambao matokeo yalishindikana kutangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa wakati kwa kuwa inasemekana mgombea wa urais wa CUF Maalim Seif alikuwa amemshinda Dr. Salmin Amour.

Kisa maarufu sana hiki.

Hii ndiyo siku nilimuona Baraka Shamte kwa karibu kwa mara ya pili.

Jana yake alipita Malindi na mimi na wenzangu tulikuwa pale ambako ndipo kilipokuwa kijiwe chetu cha kufuatilia uchaguzi na nikaonyeshwa lakini Baraka Shamte alipita kinyonge sana kwa kuwa taarifa zilikuwa zimeenea Zanzibar yote ni kuwa Maalim Seif kashinda uchaguzi.

Siku ile yote CCM walionekana mitaani wamepwelewa wanyonge wamejikusanya katika vikundi vidogo vidogo wanatafakari.

Jamaa wa Kizanzibari niliokuwanao pale wakaniambia kuwa unyonge ule wa Baraka Shamte unathibitisha kuwa CCM hakika imeangushwa Visiwani.

Wakanieleza kuwa Baraka Shamte ana nguvu kubwa ndani ya CCM na wanamtumia sawa na mbwa mkali ambae akiamrishwa, ''kamata yule,'' basi jua mbwa atakuingia maungoni na atakurarua na huna lolote la kumfanya.

Huyu ndiye Baraka Shamte.

Siku chache zilizopita ghafla katika mitandao ya kijamii anaonekana Baraka Shamte kada wa CCM wa kutegemewa anazungumza maneno makali ya kutisha.

Ukisoma ''comments,'' za wasomaji kuhusu Baraka Shamte kila mtu anamuuliza mwenzake, ''Kimetokea nini?''

Hakuna mwenye jibu.

Kukawa na ukimya hata kutoka CCM na kwa washabiki na wapenzi wake.

Bila shaka na wao pia walikuwa wamepigwa na butwaa.

Kimempata nini huyu kada mashuhuri wa CCM?

Ghafla zikaanza kurushwa ''clip'' wapenzi wa CCM wanazungumza kujibu mapigo na kauli zao hazikuwa nyepesi.

Haukupita muda ikawekwa picha Baraka Shamte yuko mikononi mwa Polisi anaonyeshwa askari kamkamta kwa staili inayofahamika kama '' Chicago.''

Hii ni staili ya ukamataji wa kudhalilisha.

Askari anapitisha mkono wake sehemu ya mbele ya suruali anaivuta juu ikawa suruali inapanda na kufanya aliyeshikwa hivi atembelee vidole gumba.

Msomaji anaweza akauliza kwani kuna ukamataji wa staha?
Naam upo ukamataji wa heshima.

Askari anaweza akakueleza kuwa amekuja kukukamata kwenda kituoni bila hata ya kukugusa na mkaongozana kwa amani na kistaarabu hadi kituoni.

Nilijisikia vibaya kumuona Baraka Shamte katika hali ile kwani kwa hakika alikuwa kafedheheshwa.

Baraka Shamte ametunukiwa Medali ya Mapinduzi.

Hii ni heshima kubwa sana ambayo hata viongozi wenyewe wa mapinduzi baadhi yao hawajapewa hadi hii leo.

Baraka Shamte ni mtoto wa Mohamed Shamte aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Zanzibar ambae serikali yake ya mseto wa ZNP/ZPPP ilipinduliwa na ASP.

Baraka Shamte alimpinga baba yake waziwazi bila kificho na hii ni moja katika historia ndani ya historia ya mapinduzi.

Baada ya mapinduzi baba yake alisafirishwa bara na kufungwa Jela ya Ukonga kwa miaka mingi.

Nimemuhoji Baraka Shamte katika kipindi cha televisheni mahojiano ambayo mimi mwenyewe nimeyapa jina, ''Mahojiano ya Wendawazimu Wawili.''

Bahati mbaya kipindi hiki hakijarushwa sasa miaka 10 imetimu.

Baraka Shamte hakunimezea mate kwa maswali yangu nami sawia niiamua iwe nipe nikupe. tukilipana kwa fedha zetu wenyewe, Waingereza wanasema, ''Pay by your own coin.''

Marehemu Mohamed Shamte alijaaliwa watoto wengi na wote ''brilliant,'' wawe wanawake au wanaume.

Baadhi yao nimefahamiananao kwa karibu sana.

Baraka Shamte si mjinga ni mtu anaejua mambo na mimi kanijua toka mapema asubuhi na kabla tunaanza mahojiano.

Historia ya Zanzibar anaijua na ipo wenye ncha ya vidole vyake vya mikono.

Nimehuzunishwa na picha ya Baraka Shamte amepigwa amefungwa bandeji ya mguu. yuko nyumbani kwake anajipumzisha.

Nalikumbuka lile pambano letu na maneno niliyoyasikia kutoka kwake vipi akiyasifia mapinduzi kwa kuleta haki na maendeleo Zanibar.

Haikunipitikia kuwa ipo siku Baraka Shamte ataishia hivi kuwa atapigwa kama walivyopigwa wengi wengine wanaodhaniwa ni wapinga mapinduzi.

Lakini Baraka Shamte si mtu mdogo kuwa kipigo chake kiwe sawa na kipigo cha Ismail Jussa kuwa kipite tu.

Kipigo cha Baraka Shamte baada ya kupigwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetoa tamko la masikitiko kuhusu kipigo hicho.

SMZ imesema katika tamko lile kuwa haihusiki na kipigo cha Baraka Shamte mzee wa miaka 83.

Haya ni mapya.
Huwa hakupatikani kitu kama hiki.

Ton Ton Macoute wa Haiti hupiga kisha wakaondoka.

Mazombie wa Zanzibar haikadhalika.

Ton Ton Macoute wao wanaingia kimya kimya wamevaa miwani ya jua hata kama ni usiku wa manane.

Wanakupiga na wanaondoka kimya kimya.

Lakini hii ni dunia ya ''improvesation.''
Ton Ton Macoute wana kitu cha kujifunza kutoka Zanzibar.

Mungu hakunyimi kila kitu.

Picha ya Baraka Shamte akiwa kavishwa bandeji binafsi narudia kusema tena imenisikitisha kupita kiasi.

Picha hii imeingia mitandaoni pamoja na taarifa kuwa Baraka Shamte kafukuzwa uanachama wa CCM.

Kisonge itapwaya kidogo.

Shida sana kupata mtu mwenye ujuzi na uzoefu aliokuwanao Baraka Shamte.

Ujuzi kama huu huwa si wa kumfunza mtu.
Mambo haya huwa ndani ya damu na ni kipaji maalum.

Historia ya Baraka Shamte imeongeza kitu mfano wa yale ya, ''The Rise and Fall...'' yaani ''kupanda na kushuka.''

Historia imejaa watu kama kaka yangu Baraka Shamte.

PICHA: Mazungumzo na Baraka Shamte nyumbani kwake Mkunazini, Zanzibar 2012, Baraka Shamte baada ya kipigo na picha ya tatu Ismail Jussa akiwa hosptali baada ya kupigwa katika Uchaguzi Mkuu 2020.

1655231611693.png
1655231792190.png
1655231831453.png
 
Mzee huja attach hizo picha fanya mapitio tuzione.
 
Kama Mbwahi na iwe Mbwai sisi tunakodisha visiwa kwa wageni wenye dolari.
 
Hii ina maana huyu Mzee Baraka Shamte ni mtoto wa waziri mkuu wa kwanza wa Zanzibar huru. Jambo hili la huyu Mzee litamalizwa kishikaji maana siasa za Zanzibar zinajulikana, atapozwa ili mambo yende shwari. Watoto wa viongozi wana namna yao ya kuyamaliza.


HISTORICAL SPEECH BY FIRST PRIME MINISTER OF ZANZIBAR MOHAMMED SHAMTE HAMAD DECEMBER 10,1963​



Tomorrow June 3nd , Tanzania will release the draft of the New Constitution while the aspirations of the people of the Zanzibar is self determination to have government of People of Zanzibar with full Indipendence.
There is no small voice with out representation , Listen to the Speech of First Prime Minister of Independent Zanzibar Honorable Mohammed Shamte.



Photo : Mohamed Shamte Hamadi (far right), with other prominent Zanzibari politician

Did you really have to go there, let alone remind those of us still seeking inspiration, that lack of political models leaves us holding onto to corpses for inspiration?

Did you have to be so cruel at a time when the majority of us are desperately seeking in every which way for better political models and sane leadership throughout all corners of what is left of the Zanzibar Republic?

When in reality, all that everyone of the leading politicians, post colonial vanguard and regional groups that had emerged after independence, ever wanted was to become Tanzanized versions of little Europeans aka Bwana Kubwas Nyerere at the expense of real Uhuru, freedom, better governance, justice and equity for all.

The bottom line is that, the people who ended paying the highest price and continue to do so, are the ordinary Zanzibari, given their current collective abysmal state of life 50yrs after this cold war Aka Union , as well as since Jamnuary 12 when impunity won the day

Source : HISTORICAL SPEECH BY FIRST PRIME MINISTER OF ZANZIBAR MOHAMMED SHAMTE HAMAD DECEMBER 10,1963
 
Zanzibar Prime Minister Mohamed Shamte at UN in December 1963 when Zanzibar accepted as member of the United Nation by the general council.



 
Back
Top Bottom