Baadhi ya mambo yaliyonikera hapa JamiiForums kwa mwaka 2017

notoriousic

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2016
Posts
425
Reaction score
484
Tunaelekea kumaliza mwaka wapendwa baadhi tukiwa salama, wengine wakiwa na upungufu wa viungo na wengine hatunao kabisa. Hatuna budi kushukuru.



Mada yangu ni kuhusu mambo yaliyonichefua sana 2017 humu JF hasa ya kiuandishi...
Mfano:
1. Xhule badala ya Shule
2. Hamekuja badala ya Amekuja
3. Ha2a badala ya Hatua
4. Mcba badala ya Msiba
5. Safali.......
6. ......
7. ..........



Ongezea na wewe yaliyokuchefua mpaka ukaacha kumalizia kusoma ulichokuwa unasoma.
 
Hata christmas bado wewe unawaza kuumaliza mwaka.
Ngoja kwanza mwaka uishe tukiwa salama ndio tutachangia hoja yako[emoji1321]
 
Sio katika jf pekee bali pia kwenye TV na Redioni. Sehemu ya L itawekwa R, basi kunakua hovyo hovyo tu.
 
Ngoja nimalize kutapika kwanza.
Jomonii=jamani
Ngachoka=nimechoka
Bhac=basi
Co=hivyo. Aaarghhhh natapika tena.
 
Umenichefua kwa kuyafukua Makaburi ambayo tayari tulijiandaa kuyasahau...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…