Baadhi ya maneno wanayotumia watu wa Arusha

black abdu

Senior Member
Joined
Dec 2, 2022
Posts
156
Reaction score
212
Ukiwa Chugga, utasikia misamiati tofauti sana na maeneo mengine, kama kwenye wingi wa maneno, mfano:

Maji - Mamaji
Ulaya - Maulaya
Watu - Mawatu
Zipu - Mazipu
Kikombe - mavikombe
Sahani ya pilau - Masahani ya pilau

Misamiati:
Mende - Parata
Okota - lokota
Nakuangalia - Nakudere
Ngeu - Turu
Kaa (mdudu wa baharini) - Ngala

Sarufi:
Hii miguu inaniuma - Hizi miguu zinaniuma

Vihisishi vya sauti:
Akamchapa kofi paaah!
Ameanguka puuh!
Kikombe kimeanguka kangaraa!
 
Sijasikia mama Giloo
 
Bangi+ugoro+mirungi+gongo+banana= Lugha ya ajabu
 
Hakuna rangi utaacha ona, nitakuletea container ya noma, ...
 
Bangi zimewaharibu hao watu
 
Kitu watu wanaamini tofauti na ukweli ulivyo,,, ni kuamini watu wa Arusha ni wagumu makauzu kitu ambacho sio kweli Arusha hii ina vijana ving'ast kweli kweli wapo kupiga mzinga wavivu ni walevi kupindukia wanavuta bangi sanaaaa!! Maneno mengiiiii mkwara yakutosha

Kutana na mtu kutoka kanda ya ziwa Mara, Geita, Mwanza, Shinyanga na Simiyu hawa jamaa wanafanya kazi kweli kweli ni wagumu hawana mikwara ukimzingua anafanya kitu hakupigi mikwara,, sio watu wakuongea sana japo ndio wanachukuliwa kama watu laini sana washamba,, Serikali haikukosea kupeleka kanda maalum Rorya Mara na pia inatakiwa iiangalie Geita kwa jicho la tatu Geita inahitaji pia Kanda maalumu
 
Hakuna rangi utaacha ona, nitakuletea container ya noma, ...
Ha ha haaaaa! Nipo katika daladala to Ngaramtoni. Nasoma comment hii na konda anatamka sentensi hii "nitakuletea kontena ya noma"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…