Baadhi ya maneno ya mpoki KTMA yaliyozua gumzo mitaani

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Ukiachana na burudani kutoka kwawanamuziki mbalimbali kwenye hafla yakukabidhi tuzo za muziki za Kilimanjaro,burudani zaidi ilikuwa ni maneno kutokakwa MC ambaye pia ni mwigizaji sanaa yavichekesho Mpoki ambaye alikuwaanawakonga nyoyo waliohudhuria kwa kaulizake tata ambazo zilikuwa zinawavunjambavu.

Na hizi ni baadhi ya kauli na misemo ambayo iliwavunja watu mbavu.Tusiaandikie penseli wakati Penny aliyekuwa wa Diamond yupo. Kama usiku wa jana ulilala na haukuota basi leo lala na mbolea utaota. Big up kwa wasichana wote ambao wamevaa vimini kwa sababu walijua kuwa Mlimani city hakuna mbu, ahsante sana kwa kwenda nawakati. Wema mamaa magazeti kuchuna buzi na kuchanganya mabwana nikipaji pia. Ukiona panya anakatisha katisha sebuleni ujue anataka kujulikana. Kirefu cha HIV ni Hatari Imeingia Vitandani. Hivi ukiwa mcheza shoo lazima ujichubue? Na mimi pia ni dokta lakini wa magonjwa ya kike.
 
Mmh ila maneno yke mengine yaliwakera na kuwadhalilisha watu kwa kweli alikosa heshma na staha waliyostahili baadhi ya wahudhuriaji
 
Mngoni wa kwanza kuzaa na mzungu!
Khaaaaaaaaa
 
Jose Mara: Nilikuwa naishi Kimara sahivi nimehamia Mbezi Beach jirani na mkuu wa majeshi

Mpoki: Unaishi Mbezi Beach umejenga?
 
Jose Mara: Nilikuwa naishi Kimara sahivi nimehamia Mbezi Beach jirani na mkuu wa majeshi

Mpoki: Unaishi Mbezi Beach umejenga?

Aaaah hili Jamaa is too clever ,

Mpoki ni mwalimu wa elimu ya mitaani.
 
Watu humu wanawaponda sana maceleb wa bongo. .lakini mpoki kufikisha ujumbe kwa njia ya utani imekuwa kero kwao
..
 
Huyu dada akizaa na mimi lazima tuzae usiku mnene......DJ Bonny Love ni bahili kupitiliza...yuko tayari kuvaa kanzu isiyo na mifuko ili asiombwe hela...(Bonny jicho lilipomtoka akapewa nyingine...) ...kama kamaindi vileeeee....
 
Unakaa na mzungu miaka mitatu hajakupeleka ulaya.
Mzungu gani anajua bei ya bajaji na anaenda sokoni halafu anakaa Mwananyamala.
Halafu Isha Mashauzi alivyopanda kupokea tuzo yake wakati wanashuka akawapa kitu "kesho asubuhi hawa wa wadada ukikutana nao lazima utawapa shikamoo"
Mpoki noma sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…