Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Ndugu yenu katika pitapita zangu nikajikuta nimeibukia Wilayani Kilombero Mkoa wa Morogoro, nilichokutana nacho kwa baadhi ya Mama Lishe ni hali ambayo inaweza kuwa hatari sana kwa afya za Watu.
Mama Lishe wa Ifakara maeneo ya Mjini hasa Mtaa wa Nduna hawazingatii usafi jambo ambalo linaweza kuwa na athari katika kuchangia maambukizi ya magonjwa ya tumbo pamoja na Kipindupindu, pia mazingira.
Nilichobaini ni kuwa wengi wao hawana vifaa vya usafi, vyombo ambavyo vinatumiwa kwa ajili ya chakula vinawekwa katika mazingira machafu, sehemu zao za kupikia pia hazijasafishwa.
Wakati hali ikiwa hivyo, Uongozi wa Halmashauri naona wapo kimya kama hawaoni vile kinachoendelea, mpaka magonjwa ya mlipuko yatokee ndiyo wataanza kuhaha kusimamia usafi wa Migahawa hiyo.
Tukumbuke hivi karibuni wenzao wa Mbeya wamekuwa na wakati mgumu kama ilivyo kwa Simiyu kutokana na Kipindipindu, wanasema mwenzako akinyolewa...
Mwanongwa nawakumbusha tu kinga ni Bora kuliko tiba.