Wakuu Naombeni ushauri katika jambo Moja :-
Kumekuwa na mazoea kwa baadhi ya Mikoa yetu TZ, ukienda kufanya biashara au kampuni, support inakuwa ndogo bcoz sio mzawa wa eneo Lile au mkabila wa pale.
Hasa Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro (Samahani )
Naombeni maarifa yenu, unawezaje kutoboa biashara/Kampuni katika Mikoa kama hiyo !?
[emoji22][emoji22][emoji22]
Mikoa ya aina hiyo huwa mara nyingi ni kwasababu ya kuwa ni jamii ya watu wa aina moja au watu wachache hivyo wanakuwa kama hawajiamini na hiyo wanafanya kujilinda wakiamini umekuja kuchukua chochote kwao.
Unatakiwa kuwa na subira nao na kuwapa offer ya vitu ambavyo wao wanapendelea au adimu sana kuvipata baada ya muda wakishakuamini wewe utakuwa miongoni mwao na watakukubali na watanunua kwako.
Hii hali ilikuwapo sana pale Moshi kuanzia miaka ya 2010 kurudi nyuma. Ila kwa bahati nzuri tokea vyuo vifunguliwe kama ushirika, mweka, na vinginevyo, vimechangia movements za wafanyabishara wadogo wadogo maeneo yale na kufungua sana biashara hadi wenyeji nao wameanza kuchangamana na wageni bila shida.
Kipindi cha nyuma ilikuwa ni mziki hata kupata chakula pale moshi maana wakazi wake wanajua kupika mtori na supu tu, hakuna kingine wanachopika.
Maduka yanafunguliwa kwa masaa yaani saa kumi na mbili hadi saa moja halafu wanafunga hadi saa saa tano asubuhi hadi saa saba then ndio imetoka hiyo hadi saa kumi na moja jioni hadi saa mbili usiku kisha hapo hautapata tena huduma ya duka hadi kesho saa kumi na mbili asubuhi.
Ila kuanzia miaka ya 2012 huku ikawa wamekuja wakazi kutoka mikoa mingine kufungua maduka Moshi ndipo tukawa tunapata huduma za maduka saa 24 ndipo wenyeji nao sasa wakaanza fungua maduka muda wote, mini super market zikafunguliwa ikawa ni uhakika wa huduma tunapata.
Migahawa na mama ntilie ikaongezeka na wapishi wa kutoka huko tanga wakaja kuwafundisha wachaga kupika ikawa uhakika wa kupata vyakula vizuri tofauti na zamani chapati hakuna, maandani ya ajabu, yaani ukitoka nje kutafuta vitafunwa unapata ndizi za kukaanga, basi labda uende town kule mbuyuni au stand ndio utapata mikate, keki, na maandazi.