kante mp2025
JF-Expert Member
- Nov 11, 2022
- 631
- 1,192
Mwanzo nilikuwa muumini mkubwa wa hawa wa kuitwa motivational speakers ilikuwa haipiti siku sijasikiliza mausia yao kuhusu maisha hasa hasa mbinu za kupata utajiri na kufikia malengo maishani.
Sikuishia kuwasikiliza tu nilienda mbali zaidi na kuyaishi maneno yao maana hawa jamaa wana principle za kila kitu, wapo wakukushauri kuhusu ndoa, kufaulu darasani,kupata mchumba, kuepuka madeni n.k
Hitimisho nimegundua hawa jamaa ni wagonga ulimbo tu nao wanajitengenezea kipato kama wagonga ulimbo wengine kupitia nakala zao na video zao pale mjini youtube.
Nimefanya utafiti nikagundua kwenye kufanikiwa kila mtu ana mbinu zake hakuna formula moja kama hawa motivesheni spika wanavodanganya umma
Ukienda huko mjini tiktok madogo wa 2000 wana washauri wao kuhusu maisha na huwaambii kitu kuna mmoja wanamuita chief god love ndio mshauri wao kuhusu mafanikio😂
Mafanikio ni fumbo wagonga ulimbo tuzidi kupambana kwa njia zetu hawa mamotivesheni spika ni matapeli kama wa tuma kwa namba hii