Tetesi: Baadhi ya sehemu na miradi tutumie majina mahalia.

mfungwa

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2015
Posts
1,291
Reaction score
342
"Stiegler" jina la kijerumani, na kikoloni na leo linatumika hata katika mpango wa umeme "stiegler's gorge" na hata kulipa umilikishi wa sehemu kwa stiegler's hivi hakuna majina ya kitanzania hadi muuite hivyo. Ebu tuacheni fikara potovu tuite jina halisi la kwetu. Hilo neno naimani hata Magufuli hawezi kulitamka vizuri. Kwanini mnataka kumsumbua hata rais wetu kutamka hadi aume meno wakati kuna chakula cha kutosha kwa sasa. Tafadhari badilini jina fasta hata kama iweje. Ifuatwe mila na desturi zetu.

Nawakilisha.
 
"Nawakilisha"....sema nawasilisha ndio sahihi zaidi


ANYWAYS WAZO ZURI MKUU
 
Hata hili ziwa Victoria kuna umuhimu wa kulibadili jina pia na Bismark rock kwa huku Mwanza.
 
Bado tuna utumwa WA fikra sijui Nani WA kutukomboa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…