Baadhi ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Wilaya ya Ilala

Baadhi ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Wilaya ya Ilala

Joined
Apr 11, 2024
Posts
24
Reaction score
55
Miongoni Mwa Mafanikio Ya Mheshimiwa Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan Katika Wilaya Ya Ilala

12819202-3977-45CB-97E1-19D5C65B93A2.jpeg
- Ujenzi wa Barabara Ya Mwendokasi; Katika Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kumetekelezwa Ilani Ya Ujenzi wa Barabara Ya Mwendokasi Inayoendelea Kujengwa Ili Kupunguza Kero Ya Usafiri Kwa Wakazi wa Wilaya Ya Ilala Na Mkoa wa Dar Es Salaam Kwa Ujumla

- Ujenzi wa Madarasa Na Maboresho Ya Shule Za Serikali Kwa Ngazi Zote. Kwenye Wilaya Ya Ilala, Shule Za Serikali Zimefanikiwa Kuboreshwa Na Kuongezwa Madarasa Ili Kukidhi Idadi Ya Wanafunzi.... Miongoni Mwa Shule Zilizojengwa Na Kuongezwa Madarasa, Ni Pamoja Na Shule za Kata Kwenye Kata Mbalimbali za Wilaya Ya Ilala

- Ongezeko La Ufaulu Kwa Wanafunzi Wa Shule Za Serikali. Shule za Serikali Zimeongeza Ufaulu Hususani Kwenye Shule za Msingi, Ambapo Shule za Serikali Zimefanikiwa Kufanya Vizuri Ukiachilia Idadi Kubwa Ya Wanafunzi Wanaosoma Kwenye Shule Hizo... Hii Inaonesha Uwepo wa Hamasa Kwa Walimu, Na Inatia Imani Na Kuinua Heshima Ya Walimu Katika Ufundishaji

- Maboresho Ya Sekta Ya Afya Kwa Kuongeza Majengo Ya Hospitali, Ujenzi wa Vituo Vya Afya, Pamoja Na Urejeshi wa Bima Ya Toto Kadi Kwa Watoto. Kwenye Wilaya Ya Ilala, Kumejengwa Hospitali na Vituo Vya Afya Kwenye Maeneo Mbalimbali, Ili Kufanikisha Upatikanaji wa Huduma za Kiafya Kwa Wananchi Kwenye Maeneo Yao... Hii Imechochea Urahisi wa Matibabu Kwa Wananchi. Lakini Pia Wilaya Ya Ilala Ni Miongoni Mwa Wilaya Yenye Watoto Wanaotegemea Bima Ya Toto Kadi, Ili Kuwapa Nafuu Wazazi Katika Matibabu Ya Watoto Wao

- Ukamilisho wa Ujenzi wa Reli Ya Treni Ya Umeme (SGR). Wilaya Ya Ilala Ni Wilaya Yenye Neema Ya Kuwa Senta (Center) Ya Mkoa wa Dar Es Salaam, Na Miongoni Mwa Miradi Mikubwa Ya Kitaifa Iliyopo Kwenye Wilaya Hii Ya Ilala, Ni Pamoja Na Mradi wa Treni Ya Umeme (SGR), Ambayo Ukamilisho wa Ujenzi wa Reli Hii, Imeinua Hadhi Ya Wilaya Ya Ilala, Na Kuchochea Maboresho Ya Miundombinu Kwenye Wilaya Ya Ilala

- Uwepo wa Miradi ya Kuboresha Elimu Katika Wilaya Ya Ilala, Ukiwemo Mradi wa (Secondary Education Quality Improvement Project - SEQUIP), Ambapo Moja Ya Matokeo Ya Mradi Huo Ni Pamoja Na Ujenzi wa Shule Ya Sekondari Ya Bweni, Mvuti... Iliyopo Kata Ya Msongola - Jimbo La Ukonga.... Ambapo Mradi Huo Umechochea Ujenzi wa Shule Hiyo Na Kutegemewa Kuwa Nafuu Ya Wazazi Kupeleka Watoto Wao Shule za Bweni.

- Maboresho Ya Miundombinu Kwenye Maeneo Korofi. Na Ujenzi wa Miundombinu, Mfano; Barabara Na Vivuko. Ambapo Baadhi Ya Maeneo Yamejengwa Madaraja na Vivuko, Ujenzi wa Barabara Kwa Kilomita Tofauti Tofauti, Pamoja Na Maboresho Kwenye Maeneo Korofi... Haya Yamefanyika Kwa Lengo La Kutatua Changamoto za Miundombinu Kwa Wakazi wa Wilaya Ya Ilala

- Maboresho Ya Maeneo Yenye Fursa za Kiuchumi. Hii Ni Pamoja Na Uhalisia wa Wilaya Ya Ilala Ambapo Ni Wilaya Yenye Mazingira Ya Kuhamasisha Fursa za Kiuchumi, Ambapo, Kumekuwa Na Maboresho Ya Maeneo Ya Biashara, Mfano Karume, Ujenzi na Maboresho Ya Masoko, Maboresho Ya Maeneo Ya Machinjioni (Vingunguti), Kuendelea Kwa Maboresho Ya Mnada (Pugu) Na Kadhalika, Ili Kuwahamasisha Wafanyabiashara, Machinga Na Watafuta Riziki Wengineo Kuwa Kwenye Mazingira Rafiki

- Uwepo wa Waajiriwa Wapya wa Serikalini Kutoka Wilaya Ya Ilala. Wilaya Ya Ilala Imefanikiwa Kuongeza Idadi Ya Waajiriwa Wapya wa Serikali, Huku Wengine Wakiwa Ni Wanufaika wa Kujiendeleza Kiuchumi Kupitia Miradi Inayoendeshwa Na Serikali Katika Utekelezaji wa Ilani

- Uhai wa Chama Cha Mapinduzi. Hii Ni Kutokana Na Ongezeko La Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Katika Wilaya Ya Ilala, Unaochochea Chama Cha Mapinduzi Kuwa Hai, Lakini Pia, Kuchochea Kukua Kwa Hamasa Ya Ushindi Kwa Chama Cha Mapinduzi

Hii Ni Miongoni Mwa Utekelezaji wa Wazi Alioufanya Mheshimiwa Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan Katika Uongozi Wa Awamu Ya Sita, Kwenye Wilaya Ya Ilala

Naomba Kuwasilisha ✍️

Wenu Katika Ujenzi wa Taifa,
Janeth Thomson Mwambije
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Mkoa - Wilaya Ya Ilala - UVCCM - DSM 🔰

KAZI IENDELEE 🇹🇿
 

Attachments

  • 03AA85F4-C026-4C4E-B249-6B9D85639C3A.jpeg
    03AA85F4-C026-4C4E-B249-6B9D85639C3A.jpeg
    791.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom