Baadhi ya Vijana CHADEMA wamtaka Mbowe kujiuzulu; kesi ya ugaidi inamuondolea sifa ya kuwa kiongozi wa kisiasa

Baadhi ya Vijana CHADEMA wamtaka Mbowe kujiuzulu; kesi ya ugaidi inamuondolea sifa ya kuwa kiongozi wa kisiasa

Chee4

Member
Joined
May 17, 2021
Posts
35
Reaction score
125
Hivi karibuni tumeshuhudia wimbi kubwa la vijana wa CHADEMA nchini wakitofautiana kabisa na mawazo ya mwenyekiti wao wa Taifa, hii inakuja baada ya vijana hao kuona kuna haja ya Chama hicho kuanza kujitafakari chenyewe kwanza kabla ya kuanzisha vuguvugu la kudai katiba mpya ya nchi nzima. Suala hilo limekuja baada ya kuona mapungufu mengi ndani ya katiba ya CHADEMA ambayo ndiyo inayoongoza chama hicho chenye siasa za uanaharakati nchini.

"Kama katiba yetu wenyewe inaminya demokrasia kuna haja gani ya kuendelea na mapambano ya kudai katiba mpya ya nchi?, angalia jinsi ambavyo muda wa viongozi wetu usivyokuwa na mpangilio ndani ya katiba yetu wenyewe, lakini angalia kwa Karibu jinsi ambavyo uhuru wa kuhoji unavominywa ndani ya chadema sasa kama ndivyo hivyo kwanini tuendelee kupambana na mahitaji ya katiba mpya wakati kwetu kupo vibaya? Nashauri chama chetu tujitazame upya sisi wenyewe halafu ndipo tuwaambie watanzania kuwa kwasasa tunahitaji kitu kingine "* wamesema vijana hao katika mkutano na waandishi wa habari mkoani Mbeya.

Vijana wa chadema kutoka mikoa kadhaa hapa nchini wakiwemo vijana wa vyuo na vyuo vikuu wameanza kutilia mashaka makubwa harakati zinazofanywa na chama chao katika hatua za kudai uundwaji wa katiba mpya hasa yakiwemo malengo mfu yanayopiganiwa na chama hicho likiwemo suala la kutaka kushika hatamu ya nchi badala ya kuomba katiba itakayoweza kuwasaidia watanzania wote ambao kwasasa haoneshi hitaji la katiba nyingine ila wanacho hitaji kwasasa ni kuona uboreshaji mkubwa wa miundombinu wezeshi ya kiuchumi, huduma za afya, uwepo wa maji safi na salama, pamoja na utatuzi wa changamoto mbalimbali za njia za uchukuzi ambazo ndizo zinazochochea ukuaji wa uchumi katika taifa letu.

Hivyo sasa chadema kuanzisha harakati za madai ya katiba mpya bila kuangalia changamoto zinazowakabili wananchi kwasasa wanakiuka haki ya mtanzania ya kupata maendeleo lakini zaidi chadema wanaonesha kutanguliza masilahi yao mbele na kuacha masilahi mapana ya watanzania jambo ambalo vijana wa chama hicho wameona ni kama hujuma fulani zinaendelea ndani ya chama hicho kupitia viongozi wao wa kitaifa.

Kukosa uzalendo kunakooneshwa na mwenyekiti wa CHADEMA taifa na kundi lao umejidhihirisha mapema sana pale alipooanza kupingana na ombi la mh Rais Mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa watanzania kuwa anania ya mabadiliko ya katiba mpya lakini kwasasa anaomba ajenge uchumi kwanza kutokana na shambulio kali la UVIKO-19 unaondelea kuyatesa mataifa yote duniani, ombi hilo la mh Rais lilipingwa vikali sana na viongozi waandamizi wa chama hicho jambo ambalo limeibua maswali mengi na mjadala usio na ukomo wa namna ambavyo CHADEMA wamekosa uzalendo kwa Taifa na kuangalia zaidi fedha na misaada wanayopatiwa kutoka kwa wahisani wao huku wakiwa wamesahau kabisa kuwa kuna wananchi wanaumia kwa ukosefu wa huduma za kiuchumi, kijamii na kiafya katika maeneo mengi.

Vijana wa Chadema wanamtaka mwenyekiti wao kuachia ngazi mara moja kwasababu amekosa sifa za kuongoza chama hicho chenye mlengo wa kati chenye mfumo wa kiliberari hapa nchini.

"Sisi kama vijana tumechoshwa kabisa na matukio yanayoyafanywa na mwenyekiti wetu amekuwa ni mtu wa kesi muda wote, sasa kwa kipindi anakabiliwa na kesi kubwa ya Ugaidi hii ni kesi mbaya sana ambayo ni zaidi ya jinai hivyo tunamuomba ajiuzulu huko huko aliko gerezani ili kukisafisha chama chetu kwa umma wa watanzania" walisema vijana wa chadema katika mkutano na waandishi wa habari mkoani Mbeya.

Uzalendo kwa nchi ni jambo la msingi sana ambalo kila Mtanzania anapaswa kuwa nalo kwasababu ya kuimarisha mshikamano, ulinzi na usalama wa nchi yetu pastokee mtu awaye yoyote yule anaanza kuangalia masilahi yake mbele na kuacha masilahi ya Taifa hakika huyo hatakuwa mwenzetu na dawa yake ni kumtenga na kumuweka pembeni na shughuli za wananchi, hivyo kwa nia njema kabisa na kulinda masilahi mapana ya watanzania CHADEMA wanapaswa kujitafakari sana kuhusu vipaumbele vya Taifa na wananchi wasiangalie wao kesho watakuwa wapi na kuacha mamilioni ya watanzania wakiteseka kwasababu ya ulafi wao wa madaraka wanapaswa kuwa na heshima kwa watanzania na kwa serikali yao na siyo kuangalia matumbo yao.
 
Ni jambo la kutia aibu na kushangaza kuona chama chenye wasomi wakubwa kama chadema, kinaongozwa na mtu alieishia darasa la nne. Ndio maana prof Safari na Mabere Marando waliamua wajitoe, kuliko kuendelea kutumiwa kwa masilahi ya mtu aliekimbia shule.
 
Mtavaa ngozi za chui mpaka lini?
Mungu huwa hamuhifadhi mnafiki hata siku moja.mbinu mnazotumia mnazidi kuimarisha upande mmoja bila kujua kuwa mnabomoa kwenu kwa mikono yote.
Hayo matakataka yanayovaa ngozi ya chui ni product ya mikesha ya mwenge. Huyo Chee4 ni mfano halisi wa hayo matakataka ya Lumumba wala hakuna haja ya kuhangaika kum-quote. Hapo anaona ametoa bonge la point kumbe bure kabisa. Kaniki ni kaniki tu hata ukiifua kwa OMO!
 
Mtu ukiamua kuandika upumbavu,huku ukijua kabisa kuwa ni upumbavu,basi tunaomba usiuandike mreeefu!! Andika mfupi tu kwa matumizi yako binafsi maana hapa hakuna mwenye haja na upumbavu wako! Sawasawa?
 
Wewe bangi haitakaa ikutoke kichwani, unaandika takataka humu badala ya kujiajiri unabaki kutegemea handouts mnayopewa kwa kuandika upumbavu mwingi humu. Very stupid.
 
Mtu ukiamua kuandika upumbavu,huku ukijua kabisa kuwa ni upumbavu,basi tunaomba usiuandike mreeefu!! Andika mfupi tu kwa matumizi yako binafsi maana hapa hakuna mwenye haja na upumbavu wako! Sawasawa?
Jamaa kajamba halafu anajinusa,hakujua majirani wanajua tangu utoto no kikojozi na kujamba.Mpuuzi sana Hugo mwandishi
 
CCM na UVCCM bado mna siasa za kishamba na maji taka zile za enzi za mwenda zake. chadema bado wako imara na Mbowe ataendelea kuwa mwenyekiti na haita fika mwezi wa9 serikali itamwacha huru kwa aibu sana
 
Mtu ukiamua kuandika upumbavu,huku ukijua kabisa kuwa ni upumbavu,basi tunaomba usiuandike mreeefu!! Andika mfupi tu kwa matumizi yako binafsi maana hapa hakuna mwenye haja na upumbavu wako! Sawasawa?
Hawa jamaa ni takataka kabisa.
 
Tuhuma hizo mnazotoa dhidi ya Mh.Mbowe ni copy and paste toka script ya CCM tangia kabla ya Hayati Magufuli.Madai yale yale kuwa Mwenyekiti wa CDM anang'ang'ania madaraka.Je,hilo linatosha kumfanya yeye na viongozi wenzake kutokudai/kuhitaji Katiba ya Tanzania?

Vijana waloitisha Press in sequence kwa hoja zinazofanana ni wana CHADEMA kweli?Mimi nawaona kama mamluki kwa sababu kama ni wanachama wa CDM walitakiwa kulaani kwanza ukamataji unaokiuka Sheria wa Mh.Mbowe na wenzake.

Pia wangejishughulisha kuhakikisha Haki inatendeka kwa wote.Kama Mh.Mbowe anao uchu wa madaraka,vipi kina Mwenyekiti Pambalu,Dr Lwaitama,Askofu Mwamakula nk nao wanastahili kushikiliwa kwa mtindo ule?Mh.Mbowe kudai Katiba na uwajibikaji wa serikali kuna uhusuano wowote na kesi alizofunguliwa?Anaadhibiwa na serikali ya CCM kwa niaba ya wana CDM?JE,hao vijana wamefurahia hali inayoendelea ya manyanyaso anayopitia Mwenyekiti Mbowe nao wanashangilia uminywaji wa Haki?Leo kwa Mbowe kesho.

Katiba tunayodai ni Mkataba kati ya Wananchi na watawala.Siyo ya vyama vya siasa na huduma za Maji,umeme,barabara,Afya au Elimu siyo mbadala wake.Katiba ndiyo kichocheo cha maendeleo na si kinyume chake.Fungueni macho vijana,Katiba bora INA manufaa makubwa zaidi kwenu kuliko kwa Mh.Mbowe,Dr Lwaitama au Askofu Mwamakula kwa sababu ya hata umri wao tu.Hatudhani kama wa natamani madaraka yoyote kupitia Katiba wanayoipigania.
 
Aibu ya mwaka.CCM bado mnafanya yale yale ya mwaka jana na juzi.Wanaomshambulia Mbowe wakichunguzwa mmoja mmoja ni walewale wa kijani.
Acha ujinga.
Hao walioyasema hayo ni kundi la vijana wasomi wanachama wa chadema waliopata maono na kutambua ulafi wa viongozi wa juu wa chama hicho ambao wao hawapambanii maslahi mapana ya Taifa na wananchi wengine bali matumbo yao tu.

Mimi sioni kitu cha msingi na cha faida kwa Taifa ambacho Mbowe anakipigania zaidi ya madaraka ambayo kamwe hatakaa ayapate.Acha kwanza wampumzishe huko lupango ili amani itamalaki nchini.
 
mbowe sio mwanasiasa ,Yule jamaa mi nilishasema ni dalali...
 
Mmeshindwa kila kona, msada wenu ni polisi na Samia dikiteita. Mbowe is here to stay labda mukamuulie jeela kama mnavyopnga. Timiza hilo basi.
Hivi karibuni tumeshuhudia wimbi kubwa la vijana wa CHADEMA nchini wakitofautiana kabisa na mawazo ya mwenyekiti wao wa Taifa, hii inakuja baada ya vijana hao kuona kuna haja ya Chama hicho kuanza kujitafakari chenyewe kwanza kabla ya kuanzisha vuguvugu la kudai katiba mpya ya nchi nzima. Suala hilo limekuja baada ya kuona mapungufu mengi ndani ya katiba ya CHADEMA ambayo ndiyo inayoongoza chama hicho chenye siasa za uanaharakati nchini...
 
Back
Top Bottom