Baadhi ya viongozi wa Simba wanaharibu wachezaji

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Kwa Upande Wa Simba Niwe MuwAzi Kabisa Sina Imani na Huyu Mzee anaitwa HANS Pope, Nafikiri Huyu Mzee Yupo Pale Kwaajiri Ya Kuiharibu Timu. Hawa Ni Wazee ambao Umri umeenda sana na Akili Zimekwisha Kuanza Kuwatoka. Kwa Ukubwa wa Simba Na Uwezo mkubwa wa baadhi ya Viongozi Walio nao Sio Timu Ya Kuanza Kuleta Maneno maneno, Majunguu na Kuwasimanga wachezaji pale Wanakuwa Hawaja perfom kama inavyotakiwa.

Leo baada ya Mchezo nimemsikia Huyuu mzee Akiwalaumu Sana CHAMA, BWALYA na LUIS kuwa wamecheza chini ya Kiwango na Wanastahili kuwekwa Chini na Kuhojiwa na Kuonywaa, Mzee amesema Haya kwa Macho makavu kabisa huku akitoa hoja Za Kipuuzi sana kuwa Chama Kakosa Goli la Wazi Kwa Uwezo Wake Hakutakiwa Kukosa Lile Goli. Hoja Za Mzee zinaonesha Kabisa kuwa Umri umemtupa Mkono na Sisi kama Mashabiki wa Simba Tunapaswaaa kumtoa Kwenye Uongozi wa Timu. Kwasababu kwa Maneno yale kunawakatisha Tamaa wachezaji wetu wote waliopambana leo kuhakikisha Tunarudi Mchezoni.

Labda Mzee Hans Pope Nikueleze kuwa

1. CHAMA- Leo Amefanya kazi Kubwa Licha ya kukabwa sana Na Mabeki wa Yanga, Hakuna Asietambua ubora wa Chama iwe mchezaji wa Yanga Au Mchezaji Wa Simba, Hivyo kwenye Derby kama Ya Leo isingekuwa Rahisi Chama Kuachwaa Kucheza kama Anavyotaka Lazima Angepata upinzani mkali kama alivyoupata kuhakikisha kila Kitu inalinda goli lake. Mzee Nikukumbushe kuwa Hakuna Mchezaji Ambae atakuwa Bora kila Mechii kwa Miaka 2 mfululizo aisije kupata upinzani hii ipo hata kwa Kina RONALDO NA MESSI. Mzee Hans Pope Uelewe kuwa Hata Chama nae ni Binadamu kama Binadamu Wengine Walivyo. Anachotupatia chama kama Mashabikii ni kikubwa kuliko anacho tukoseaa. Kumuita kumuhoji na kumuonya ni kumvuruga na Kumtaka kumharibia kiwango chake. Kumbuka Kwenye FA ya Azam Wachezaji wa Simba Ni Wale wale lakini wa Yanga Sio Wale wale, kulikuwa na TshiShimbi na Niyonzima ambao leo hawakuepoo usitegemee Chama Acheze kama Anavyo Taka. Mzee Hana Pope Kaa chini ufikirie

2. LUIS- Hivi unaanzaje kumuita Luis kumuhoji kwa Kiwango chake cha Leo? Nani Kacheza Kama Luis Kipindi cha Pili? Luis Ndio Ambaye amefanya Wachezaji wa Yanga wote warudi kulinda Goli, Luis Ndio ametufanya Tuone Leo Tumenyimwa penalt za Bure na Faulo za Wazi kwasababu ya Uchezaji Wake unaanzaje kusema kacheza chini ya Kiwango? LAbda Mzee Hans Pope nikukumbushe kuwa Luis Ndio Alie Toa Assit ya Goli letu la Kusawasha, na Ndie alie walitaa wachezaji kuacha kushangilia na kwenda kupambana tuongeze bao, Wewe mzee na Uzee wako unakuja Kwenye media kuwa Kacheza Chini ya Kiwango ulitaka Acheze Vipi? Mzee Hans Pope tuambie?

3. RALLY BWALYA- Mzee Hans Pope Hivi huji kuwa Bwalya Hii Ni Derby yake Ya Kwanza Tofauti na Dilunga? Kitendo cha Kumuanzisha Tuu Bwalya Yalikuwa ni Makosa ya Wazi Ya Benchi La Ufundi kwasababu Bwalya ndio ameenza Derby kwa Mara ya kwanza Tofauti na Dilunga ambaye kacheza Derby Nyingi... Ulitaka Aperfom Vipi? Kiwango cha Bwalya Sio Cha Kuhoji na Kwa Pressure ya Mchezo ilivyokuwa Bwalya Sio wa kuitwa na Kuhojiwa, Mzee Hans Pope Unatukosea Mashabikii

Hukuona Uchezaji wa Bocco Ila Hao ndio uliwaona? hata Bocco Nae Sio wa Kulaumiwa Japo kakosa Magoli ya Wazi lakini ametoka majeruhiii anakutana ja Derby wakati hatuna Mtu wa nguvu kama Kagere na Mugalu.

Mzee Hans Pope Wapongeze Wachezaji Wetu leo wamepambana sanaaaa Wamepambana na Pressure za Mashabiki, Wachezaji wa Yanga na Muamuzi alisha watoa mchezo kutokea kipindi cha Kwanzaa. Acha Kuwalaumu wachezaji na kuwakatisha tamaa. Wewe mzee ndio unafanya wachezaji wafikirie kuanza kuondoka Simbaa... Tuwe wa Kweli Yanga Ya Leo sio Sawa Na Ile ya FA hivyo Mzee Hans Pope Acha kukurupuka.
 
Hans yupo sawa ila wewe umeandika kishabiki haswa penalty gani ile unataka tuanze kulalamika ovyo nasi kama pope mpira kipindi cha Kwanza tulizidiwa na kipindi cha pili wenzetu alivyo Toka moro nasi tukapata nafasi kukwenda langoni kwa mpinzani Yanga wamelenga zaidi lengo letu ova.
 
Yupo Sawa Kuwalaumu Wachezaji Walio Pambana? Hatuhitaji kulaumi hata kocha wetu Kasema, Lakini Mzee Hans Pope Kusema Wachezaji Wamecheza Chini ya Kiwango as If wanaihujumu Simbaaa Anakosea.
 
Mnaenda hatua 2 mbele, mnarudi hatua 10 nyuma
 
Hivi simba kwa nini mprira waliocheza kipindi chapili hawakuanza kuucheza toka mwanzo. Pasi fupi zilishakwama kitambo hawakubadilika mpaka wakafokewe mapumziko ndio wanakuja kucheza mpira.

Naona kama tumepoteza game kizembe.
 
Hahahaaa mwiteni mumhoji mna sheria na kanuni zenu humu haimsaidii na hana mda wakusomaa haya mautumbo
 
Tatizo muna wa-overrate wachezaji wenu wa kibongo. Mchezaji akikimbiza beki za Lipuli munamwita Mess. Mchukue Chama kwenye Derby 3 za Lig kuu uone unamweka wapi?

Ukweli ni kwamba Simba hii ni mbovu sana kuliko ile ya kina Kotei. Nyuma hakuna beki siku ikikutana na timu yenye washambulia wawili huko champions League itapigwa hata 8
 
Ya kina kotei ilikuwa na beki gani?
 
Hans Pope yuko pale kwa sababu ya pesa zake huyu ndio alimwondoa Tambwe akampeleka Yanga, yeye ndio alimwondoa uchebe inawezekana wakati mpira unachezwa alikuwa amesinzia akaamuka baada ya goli kufungwa hawa ndio walisemwa na uchebe si ajabu keshachukua pesa za kumuuza chama anatafuta sababu.
 
Ndo maana walimfanyia fitna Senzo.

Senzo hakuwapa nafasi hao wazee waongee ongeee

Uchebe alisema simba tunaongozwa na watu wasio na weledi na mpira.

Kaongea Pumba sanaa

Pumbaa kabisa aiseh

Hao ndo wazee walio mshika masikio Mo

Hao hao ndio waliotuletea BM mpiga makonzi.

Bw. Magoli pekee yako ndio naona anaweza kuongea kuliko huyu mzee.
Huyu na mwenzie kaduguda.

Nlishangaa juzi kaduguda anakwambia tuna morrison wakati huyo mtu ana adhabu yaaaaani hao ndio viongozi wetu sasa.
 
Bw. Magoli aliamua kuacha uCEO kwa Midomo chuchunge ya hao wazee
 
Simba hii ya Svensen klabubingwa aitoboi,ngoma itaishia kwenye mzunguko tu. Kama Simba hii ya leo inashindwa kuifunga Yanga yenye wachezaji 100% mazezeta ndo itawafunga wakina al-ahali na wakina Mazembe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…