BIG STONE AND CONER STONE
JF-Expert Member
- Mar 11, 2023
- 421
- 728
Wacha wee akili yao iko mbele zaidi ya mjerumani?Hao ni waajemi na sio waarabu, akili yao iko mbele toka enzi na enzi
Upo sahihi lakini pia wapo Wabulushi wa Iran. Wikipedia inasema:Waburushi ni wengine kabisa mkuu,wao kwao ni Pakistani Baluchistan huko,
Waajemi na wabulushi ni tofauti kabisa,wabulushi wana uasili na uhindi kiasi.
Asilimia 80 ya magari yanayo tumika ndani ya Iran wanatengeneza wenyewe na pia Iran ni muuzaji mkubwa wa magari kwenye nchi za Asia ya Magharibi na kati.Mbona yule mtaalam wao wa nyuklia aliyepigwa bomu na kufa kipind kile alikua anatembelea Nissan Fuga ?, hayo magari ya Iran ni kwa ajili ya kupigia pcha tu kama sisi huku na magari yetu ya Nyumbu au lile la Kipanya
Wapo pia Wabulushi wa Iran mfano Rostam, tuna muingiliano nao sana huku kwetu na nina ndugu zangu wameoa hao wabulushi. Nawajua kiasi chake mkuu.Waburushi ni wengine kabisa mkuu,wao kwao ni Pakistani Baluchistan huko,
Waajemi na wabulushi ni tofauti kabisa,wabulushi wana uasili na uhindi kiasi.
Swadakta.Upo sahihi lakini pia wapo Wabulushi wa Iran. Wikipedia inasema:
Eneo la Balochistan limegawanyika kati ya nchi tatu: Iran, Afghanistan na Pakistani. Kiutawala inajumuisha jimbo la Pakistani la Balochistan, jimbo la Irani la Sistan na Baluchestan, na maeneo ya kusini ya Afghanistan, ambayo ni pamoja na mikoa ya Nimruz, Helmand na Kandahar .[5][6] Inapakana na eneo la Pashtunistan kaskazini, Sindh na Punjab mashariki, na maeneo ya Irani magharibi. Pwani yake ya kusini, ikiwa ni pamoja na Pwani ya Makran, inasogeshwa na Bahari ya Arabia, hasa sehemu yake ya magharibi, Ghuba ya Oman.
Chanzo: Balochistan - Wikipedia
Kutokana na ramani niliyoipitia inaonesha Balochistan imetapakaa sana. Kihistoria wabulushi wametapakaa sana, wao ndiyo walikuja Afrika ya Mashariki na kuwatowa Wareno kwa nguvu, waliwatandika na kuwashinda Wareno licha ya kuwa wareno tayari walijichimbia kwenye ngome (fort Jesus) Mombasa na "Ngome Kuu" Unguja. Baada kuwatandika Wareno Waliikabidhi miji hiyo ya Mombasa na Unguja kwa watawala walioondolewa na Wareno.