Baadhi ya waajiri wana tabia ya kuomba vitu vingi sana kwa mtu alietuma maombi ya kazi

Baadhi ya waajiri wana tabia ya kuomba vitu vingi sana kwa mtu alietuma maombi ya kazi

Zero Competition

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2018
Posts
347
Reaction score
553
Kuna baadhi ya waajiri wana tabia ya kuomba vitu vingi sana kwa mtu alietuma maombi ya kazi

Mfano kuna taasisi flani waliwahi kutangaza kazi lakini kwenye usaili wanakuambia uende na barua tatu za wadhamini wakiwa wameambatanisha na barua zao za utambulisho toka serikali ya mtaa pamoja na copy ya vitambulisho vyao vya uraia

Na wewe mwenyewe muomba kazi wanakuambia uende na barua yako ya utambulisho toka serikali ya mtaa, kitambulisho cha uraia pamoja na picha za passport size mbili.

Yani vitu vyote hivyo wanaomba wakati bado hauna uhakika wa kupata hiyo nafasi na ukikosa hawafanyi uungwana wa kukuambia uende ukachukue documents zako.

Badilikeni waajiri

Msumbue mtu alete vielelezo vingi ikiwa tu tayari ushampatia nafasi ya ajira kuliko kumsumbua kwenye hatua ya awali wakati hana hata uhakika wa kupata hiyo kazi.
 
Back
Top Bottom