Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.
Palikuwa na haja ya kuwashauri baadhi ya wagombea kusitisha tu kampeni zao hasa hasa kampeni zenyewe zinapokuwa za gharama kubwa, zisizokuwa na tija na huku zikiwa hazina jipya kabisa.
Kwa mfano, wengine tangia kuzinduliwa kwa kampeni mwishoni mwa August ile mbele ya macamera lukuki ya TV stations zote zilizopo nchini, hamna jipya lolote waliosema bali ni yale yale ya kabla hata ya uzinduzi.
Jamani eeh tufanye tumesikia basi!
Maana tumenunua madege, tunajenga meli maziwani, tumejenga mahospitali na dispensaries kadhaa, tunajenga SGR, Stiggler's Gorge, nk nk. Habari ni hiyo hiyo kote wanakokwenda utadhani ni recorded CD inachezwa.
Ukizingatia kuna huyu anayeambatana na magari si ya kitoto zaidi 100 na watu wasiopungua 400 kwenye misafara yake. Huu ni upotezaji wa raslimali usio na tija kwa ajili ya kwenda kusema yale yale?!
Kwa kweli hawana jipya na hii hadithi wanayoirudia rudia kwa hakika imechokwa na imedoda vilivyo.
Kwamba tuliamua kupumzika hizi siku mbili tatu? Bora tungepumzika jumla tu. Hizi kampeni hazina tija wala manufaa hata kulinganisha na juhudi tu.
Bora kama tungekuwa na mapya labda kuhusiana na mipango kuelekea kuangazia haki au uhuru wetu. Haya mengine mbona mgombea huyu yamemletea tafrani zaidi kuliko umaarufu?
Habari ndiyo hiyo.