A
Anonymous
Guest
Serikali yetu inahimiza suala la haki, inapinga unyonyaji. Lakini hii imekuwa tofauti katika baadhi ya wahadhiri wa baadhi ya kozi za kiswahili mwaka wa tatu (CoED & Co. Of social sciences)katika chuo kikuu cha Dodoma.
- Kuna wanafunzi hawakufikisha coursework ya somo moja la kiswahili.
- Walienda kwa mwalimu kuomba alama chache zilizopungua lakini mwalimu alidai hana access kwa sasa.
- Ajabu mwalimu anamtumia Cr wa kozi hiyo kuchukua pesa kwa wanafunzi ili waongezewe alama.
- AWamu ya kwanza walitoa 50,000/= na kuongezewa alama zilizopungua kufika 16.
- Ilipobaki siku mbili kufika siku ya mtihani (UE) dau likapanda hadi 100,000/= hapo waliongezewa hadi alama 20, yaani kama mtu alikuwa na CW ya 10 inakuwa 10+20 =30(total CW)
- Jambo hili sio sawa. Wanafunzi hatupendi kuwa na carry over mwaka wa tatu ndo maana inapelekea hivyo.
- Hakuna mtu anapata nguvu ya kulisemea hili kwa sababu maisha ya mwanafunzi yapo kwa mhadhiri.. nitaanzaje kusema je likitokea la kutokea itakuwaje mtoto wa kijijini kidumu na mfagio mimi.
- Si wahadhiri tu bali wanafunzi wote wanaoshiriki hivyo sio jambo zuri.