Baadhi ya Wakandarasi Wazawa wanamuangusha Rais Samia

Baadhi ya Wakandarasi Wazawa wanamuangusha Rais Samia

FIKRA HAI

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2013
Posts
231
Reaction score
79
Kandarasi nyingi hasa za barabara zinafanywa chini ya viwango na wakati mwingine hawana hata vifaaa kwa ajili ya kazi.

Hii imepelekea adha na Usumbufu kwa watumiaji wa barabara hizi zinazofanyiwa ukabarati. Mfano kipande cha barabara kutoka Mabibo Mwisho hadi makutano na Morogoro Road.

Mkandarasi huyu Hana Vifaa, amekodi katapila ambazo ni mbovu na kila siku ni kuziba pancha. Amefukua kifusi cha mwanzo na akarudishia hicho hicho.

Barbara hii muda wingi imefungwa inamkuwa Usumbufu mkubwa kwa watumiaji. Inasemekana mkandari Mchina aliondolewa akapewa mtumishi wa TANROADS baada ya kutoa ten %.

Barabara ya Pugu Chanika kuna baadhi ya vipande vinafanyiwa ukarabati kwakutoa lami iliyochoka suala la ucheleshwaji kwakutosekana Vifaa na pengine uwezo limekuwa changamoto kubwa Sana pia kwa mkandarasi huyu.

Viongozi waliopewa dhamana kwa ajili ya masilahi mapana ya wananchi walimulike hili kwa karibu sana.
 
Back
Top Bottom