DOKEZO Baadhi ya wakuu Shule za Kidato cha tano wanatoza pesa ili kupata nafasi za kuhamia

DOKEZO Baadhi ya wakuu Shule za Kidato cha tano wanatoza pesa ili kupata nafasi za kuhamia

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Baadhi ya wakuu wa shule hasa zile kongwe na zinazofanya vizuri katika mitihani ya taifa ambazo ni za umma wamekuwa ni kero kubwa sana. Wamekuwa wakiwatoza fedha baadhi ya wanafunzi wanaotaka kuhamia kwenye shule hizo.

Baadhi yao wanawatoza wazazi shilingi Laki 1 hadi Laki 5 ili waweze kupata nafasi ya kuhamia kwenye hizo shule.

Wamekuwa wakitumia neno NAFASI ZA KUHAMIA ZIMEJAA ili kupiga pesa. Mfano wanafunzi waliopangiwa kwenda combination za arts lakini wanataka kwenda kusoma sayansi wengi wamekumbana na kadhia hii.

Vilevile wanafunzi wengi waliopangiwa shule mpya na zile zilizoko pembezoni wamekimbilia kwenye hizo shule kongwe na zilizoko mjini kwa hiyo Serikali ilitazame jambo hili kwa jicho la kipekee sana hususan TAMISEMI
 
Shule kongwe si ya kila mtu jamani, kila mzazi anapeleka mtoto pale so lazima watengeneze mazingira ya kukatisha wazazi wanaopenda vya bure.
 
Kwanini mtoto wako hakufaulu vizuri zaidi ili apelekwe huko Shule kongwee? Hakuna cha buree, toa pesa mwanao awekwe hapo.

Sasa na shule kongwe watu wanalia lia je Special? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom