Naomba namimi niweke mchango wangu juu ya majina,
Ki uhalisia sisi ni waafrica wenye tamaduni zetu, tunapaswa kufahamu ya kwamba mwanadamu anayo icon yake ambayo inapaswa kuwa tofauti na mtu mwingine yeyote,
Icon hiyo huwa ni jina ambapo jina kamili la mtu ni lazima yawe matatu
Jina lako wewe, jina la baba yako, na jina la ukoo
Jina lako yawezekana ikawa ni lile ambalo ulipewa na wazazi wako ukiwa mdogo au pengine ulilibadilisha wewe mwenyewe kisheria kwa kuapa mahakamani
Jina la kati ni lazima liwe la baba yako mzazi labda kuwe na uhuni mama yako alifanya lakini lazima jina la baba yako mzazi ndo liwe katikati
Jina la mwisho ambalo ni la tatu ni lazima liwe la ukoo ili kukutofautisha na mtu mwingine
Mfano Jerico Simon Mgaya hili ni jina pekee ambalo siyo rahisi kumkuta mwingine ana jina kama hilo
Lakini ukiandika, Jerico Simon wapo wengi tu
Au hata Jerico Mgaya wapo wengi pia
Kwa hiyo kinachotofautisha hapo ni kati na ukoo
Nije kwenye umuhimu wa ukoo
Ukoo ni muhimu sana kwa sababu katika maisha yetu ya Leo tunazunguka sana kutafuta
Leo na kesho umekutana na msichana anajitambulisha kwa majina mawili mf Angel Simon umempenda umeshamzoea kabisa binti na unawaza kwenda kujitambulisha kwao
Kumbe ni Angel Simon Mgaya ni Dada yako wewe umechelewa kumhoji vizuri hadi ushalala naye
Kuna rafiki yangu mmoja anaitwa Yocktan Jackson Hosea
Ana majina matatu kweli lakini jina la ukoo hakuna nimejaribu kumhoji hilo jina la ukoo hajui chochote
Sasa na yeye ni MTU mzima na anawatoto wake he unafikiri anao uwezo wa kuwafundisha wanae?
Kwa hiyo kumbe hata huyo Angel Simon na Jerico Simon wanaweza kuoana kwa sababu hilo jina la ukoo wote hawalitumii na hawalijui kabisa
Naomba tuwafundishe watoto wetu kuyatumia majina yetu yote matatu
Na hii ni kanuni yetu kisheria ila waliotuharibu ni waarabu wametufundisha visivyo
Ruksa kukosoa lakini siyo matusi
Asanteni
Elewa Surnames mara nyingi ni jina la ukoo mtu husika. Mf. Mboro ni ukoo
Huku Manzese Kuna jamaa anaitwa "Kundugeni"
pia maeneo ya Buza nyama choma Kuna dalali anaitwa "Khamis Nguo gani" na mwingine Mtoro wa kufikia wa ma mdogo anaitwa "Dotto Mumewangu"