Baadhi ya wanawake wazalendo wa TANU

Baadhi ya wanawake wazalendo wa TANU

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
PICHA YA BI. CHIKU BINT SAID KISUSA, BI. TITI MOHAMED, BI. TATU BINT MZEE, JULIUS NYERERE NA AKINA MAMA WENGINE

Mmoja wa wasomaji wangu amenitumia picha hiyo hapo chini ya akina mama wazalendo wanachama wa mwanzo wa TANU hao niliowataja hapo juu.

Kulia ni Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Titi Mohamed, kushoto ni Bi.Tatu bint Mzee na huyo katikati ni Julius Kambarage Nyerere.

Hii picha ilipigwa Uwanja wa Ndege wa Dar-es-Salaam akina mama hao walipokuwa wanamsindikiza Mwalimu safari yake ya kwanza UNO mwaka wa 1955.

Picha hii ni bora sana kuliko ile mliyoizoea ambayo nimekuwa nikiitumia.

Kaniletea na picha nyingine ambayo In Shaa Allah nitaiweka hapa wakati muafaka.

Namshukuru sana huyu ndugu yangu.

IMG_20210827_104805_4~2.jpg


Screenshot_20210827-112721_WhatsApp.jpg
 
Mwalimu alikuwa mvumilivu sana, Bibi Titi Mohamedi alikuwa si wa kawaida aisee!! mimi ningeanguka dhambini aisee.
 
Kaka mkubwa asante kwa kutokuwa mchoyo tumewaona wanawake hawa miamba ya kupambania uhuru wetu ambao leo una milkiwa na polisi.
 
Back
Top Bottom