Tunaomba mtusaidie kupaza sauti, Serikali ijue madudu yanayofanyika Mpanda, watoza ushuru wanaotoza ushuru wa magari makubwa kushusha mizigo na kupakia mizigo ndani ya mji sio waaminifu.
Baadhi yao wanachukua hela wanaweka mfukoni na hawatoi risiti, kati ya magari 100 wanaoweza kupewa risiti ni wahusika wa magari 10 au 15 tu, wenye magari wengine waliosalia hawapewi risiti.
Ushuru halali ni Sh 50,000 lakini wenyewe wanachukua Sh 30,000 wanaweka mfukoni kisha wanamwambia dereva “We kashushe mzigo!”
Hali hii inatokea kwa wenye magari wengi ambao wanakuwa wanashusha mizigo ya dukani, mbao, simenti, magodoro n.k
Wanaocheza michezo hiyo mara nyingi ni Watu wa magetini, anayetoza ushuru wa parking mjini pamoja na baadhi ya viongozi wao.
Mageti yako nje ya Mji kabla ya kuingia ambapo kwa barabara ya kutoka Tabora geti lipo Nsimbo, barabara ya kutoka Kigoma Kabungu na Misukumilo, kwa barabara ya Sumbawanga-Rukwa geti lipo Magamba.