- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Mtaani kumekuwa na maneno mengi sana Juu ya suala la Watu Mshono (Kidonda cha upasuaji) Kuwa wanapata Maumivu Kipindi cha hali ya hewa ya Baridi, Mvua au mawingu, Japo wapo kadhaa ambao walithibitisha kupata maumivu katika vipindi hivyo, Lakini ningependa kufahamu zaidi katika Ngazi ya Utabibu.
- Tunachokijua
- Kovu la upasuaji (mshono) ni alama inayobaki baada ya jeraha la upasuaji kupona. Kovu linaweza kuwa laini au ngumu, jembamba au pana kutegemea ukubwa wa jeraha kabla ya kushonwa, rangi yake hutofautiana kutoka kwenye ngozi ya kawaida. Wataalamu wa afya wanasema uangalizi mzuri wa kovu hili unaweza kusaidia kupunguza ukubwa wak na kulifanya lisionekane sana.
Kumekuwapo watu mbalimbali ambao wamekuwa wakilalamika kupata maumivu kwenye Kovu la upasuaji (mshono) katika mazingira ya baridi na mvua. Hoja hii imekuwa kawaida sana kwa wazazi ambao wamewahi kujifungua kwa njia ya upasuaji.
Upi ukweli kuhusu hoja hii?
JamiiCheck imefuatilia hoja hii katika vyanzo mbalimbali vya Wataalamu wa Afya na kubaini kuwa ni kweli baadhi ya watu wenye makovu ya upasuaji (mshono) hupata maumivu kwenye eneo la mshono wawapo katika mazingira ya baridi. Majukwaa mbalimbali ya Afya yakiwamo Medical News Today, Kituo cha Kutibu Majeraha cha Marekani, Marivale Hand Clinic yanakubaliana kuwa hali ya hewa ya baridi inaweza kusababisha mishipa ya fahamu karibu na mshono kukaza au kuvuta na kupelekea hisia za maumivu sehemu yenye kovu la upasuaji (mshono) au hata jeraha la zamani (kovu).
Medical News Today wanaelezea kwa ujumla wake namna baridi inavyoweza kusababisha maumivu kwenye jeraha lolote la zamani hata kama halikuwa na mshono wala upasuaji. Wachambuzi hawa wa taarifa za Afya wanaeleza kuwa hali ya hewa inaweza kuwa na athari kubwa kwenye maumivu ya mwili, hasa kwa watu walio na majeraha ya zamani au mashono ya upasuaji.
Wakifafanua zaidi hoja yao Medical News Today wanasema:
Picha kutokea mtandaoni
Wakati joto linaposhuka, tishu za mwili huanza kukaza. Hii ni pamoja na ngozi, misuli, na mishipa. Wakati tishu hizi zinakaza, inaweza kuongeza shinikizo kwenye mishipa ya fahamu, ambayo husababisha maumivu. Tishu mbalimbali hukaza kwa viwango tofauti wakati wa baridi. Kwa mfano, tishu za kovu (scar tissue) hukaza kwa kiwango tofauti na tishu za kawaida, na hivyo inaweza kusababisha maumivu zaidi kwenye eneo la jeraha la zamani au mshono wa upasuaji.
Kwa upande wao, Kituo cha Kutibu Majeraha cha Marekani hawatofautiano na Marivale Hand Clinic ambao wote wanafafanua kuwa wanaeleza kuwa hali ya hewa ya baridi inaweza kuwa na athari kubwa kwa mwili wa binadamu, hasa kwa wale walio na majeraha ya zamani au mashono ya upasuaji. Wakielezea zaidi hoja hii sehemu ya maandiko yao wanasema:
Wakati wa baridi, mwili wa binadamu hufanya mabadiliko mbalimbali ili kuhifadhi joto, mabadiliko ambayo yanaweza kusababisha mvutano wa misuli, kukaza kwa viungo, na maumivu kwa wale walio na majeraha ya zamani au mashono ya upasuaji.
picha kutokea mtandaoniHivyo, kutokana na vyanzo na ufafanuzi huo kutoka kwa wataalamu wa Afya mbalimbali JamiiCheck inaona kuwa hoja ya baadhi ya watu kulalamika kupata maumivu kwenye mshono au makovu ya zamani ni ya kweli.