Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 243
- 287
Wana JF kuna Kero moja ambayo imekuwa ikitutafuna sisi wakazi wa Kijiji cha Mshikamano, Kata ya Rusumo ambayo ni wahudumu wa Kituo cha Afya cha Rusumo kilichopo Wilayani Ngara mkoani Kagera.
Hiki kituo kilijengwa mahususi kwaajili ya kurahisisha huduma za afya kwa wakazi wa kijiji hicho na vingine vya jirani ndiyo maana kilijengwa Rusumo jirani na Boda ya Tanzania na Rwanda.
Cha ajabu ni kwamba baadhi ya Watumishi wa kituo wamekuwa wakilalamikiwa na Wagonjwa kwamba wanawatukana wagonjwa pale wanapohoji baadhi ya mambo ambayo yanaihusu hospitali hiyo, mimi pia nimethibitisha hilo mara kadhaa.
Kibaya zaidi ni kwamba, wale wahudumu wa afya ikifika siku ya Jumapili, huwa hawafanyi kazi wakati kituo wanachofanyia kazi kinaweza kuwa na hadhi ya Hospitali ya Wilaya kutokana na usanifu wa majengo yake na miundombinu iliyowekwa.
Kuna wakati nilipeleka mgonjwa pale akatolewa lugha chafu baada ya kuhoji kuhusu huduma baada ya kuweka muda mrefu bila kuhudumiwa.
Jambo lingine ni kuwa kuna tabia ya uzembe kwa baadhi ya Wahudumu wake kiasi kwamba kuna wakati wanaopeleka wagonjwa hapo huwa wanatamani kuwahamisha kwenda kwenye hospitali zingine.
Wahudumu wenye tabia hizo inadaiwa wameshawahi kuonywa kuhusu huduma mbovu wanazotoa lakini hawasikii maana mtindo huu umekuwa wa kujirudiarudia, ukifika Mapokezi, mhusika wa hapo anaweza kuendelea kuongea na simu hata kama kuna mgonjwa wa dharura, wala hashtuki hata kidogo.
Ipo haja kwa mamlaka kutoa onyo kali kwa wale Watumishi ili huduma za afya zitolewe kwa watu kama inavyokusudiwa sio kutuchezea maana kuna ndugu zetu kadhaa wameumizwa na matendo hayo.
Nategemea kuona mabadiliko kwenye hili kwakweli lasivyo hali itakuwa mbaya...