KERO Baadhi ya Watumishi wa NHIF Kibaha wajitafakari, hawana customer care nzuri kwa Wateja

KERO Baadhi ya Watumishi wa NHIF Kibaha wajitafakari, hawana customer care nzuri kwa Wateja

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Baadhi ya Watumishi wa NHIF Kibaha Mkoani Pwani huduma zao sio nzuri, pia lugha zao pia sio rafiki kwa wateja, nimeshuhudia hali hiyo mara kadhaa na Wateja wengi wamekuwa wakilalamika.

Mfano kuna mtu aliambiwa na mtumishi mmoja wa hapo “Wewe chizi nini! Kwani umezaa na baba yako...?” Kisa kulikuwa na changamoto ya jina kukosewa kwenye document zake.

Imagine huyo ni Mtumishi wa Umma anamjibu Mwananchi hivyo tena mbele za watu na ndani ya Ofisi ya Umma!

Kibaya zaidi kuna mhudumu wa kiume pale NHIF KIBAHA mwembamba mrefu, anakaa meza ya kwanza kushoto ukiingia tu mlangoni anaongoza kwa kuwajibu ovyo wateja wanaofika katika ofisi zao.

Naomba uongozi uwape mafunzo Watumishi wao kuhusu customer care, kwani sio nzuri na inakwaza.
nh.jpeg

Pia soma ~ Nimepata huduma mbovu kutoka kwa Mfanyakazi wa NHIF - Dar, imebidi Kiongozi wake wa juu aingilie na kuniomba radhi
 
Back
Top Bottom