Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Tanzania imepata fursa na heshima ya kuwa nchi mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Kuhusu Nishati (Africa Energy Summit) utakaofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 27-28 Januari, 2025.
Mkutano huo unaandaliwa kwa pamoja baina ya Serikali ya Tanzania, Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan; Marais wa Nchi za Afrika 24; wawakilishi wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Afrika 21; Wakuu wa Taasisi za Kimataifa sita (6) wakiwemo Rais wa Benki ya Dunia, Rais wa Benki ya Afrika na Rais wa Taasisi ya Rockefeller; na Washirika wa Maendeleo watano (5) watashiriki Mkutano huo.
Aidha, jumla ya washiriki wengine 2,600 wa ndani na nje ya Tanzania wamejisajili kwa ajili ya Mkutano huo.
Kufuatia ugeni huu mkubwa, baadhi ya barabara muhimu za Jiji la Dar es Salaam zitafungwa kama ilivyotangazwa na Jeshi la Polisi.
Hivyo, ili kuepuka usumbufu ambao unaweza kusababishwa na kufungwa kwa barabara hizo, Serikali inaelekeza kuwa tarehe 27 na 28 Januari, 2025 watumishi wa umma katika Mkoa wa Dar es Salaam wafanyie kazi nyumbani isipokuwa wale ambao mazingira yao ya kazi yanawataka kuwepo katika vituo vya kazi kama vile watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama, sekta ya afya na sekta ya usafiri na usafirishaji.
Vilevile, Benki hazitafungwa na biashara katika Soko la Kariakoo zitaendelea kufanyika. Hoteli na migahawa nayo haitafungwa.
Pia soma: DAR: Barabara 9 kufungwa kwa siku sita kupisha mkutano wa madini chini ya Viongozi kadhaa wa Afrika
Aidha, waajiri katika sekta binafsi wanashauriwa kuruhusu watumishi wao katika Mkoa wa Dar es Salaam kufanyia kazi nyumbani au kuweka utaratibu ambao hautasababisha changamoto ya usafiri kutokana na kufungwa kwa barabara hizo.
TAARIFA KWA UMMA

Imetolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka
KATIBU MKUU KIONGOZI
26 Januari, 2025
Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka
KATIBU MKUU KIONGOZI
26 Januari, 2025