Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linamshikilia Festo Nzuki (39), mkazi wa Kitongoji cha Izyila, Kata ya Mlowo, Wilaya ya Mbozi kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake, Jackson Nzuki (10) ambaye ni mwanafuzi wa darasa la sita, Shule ya Msingi Ivwanga kwa madai ya kutorudisha chenji ya Sh9,000 baada ya kutumwa kununua chapati.
Taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Januari 7, 2025 na kamanda wa polisi mkoa huo, Augustino Senga inaeleza kuwa, tukio hilo limetokea Januari 2, 2025 asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe.
Senga amedai kuwa, Desemba 30, 2024, Jackson alipigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na mtuhumiwa ambaye ni baba yake mzazi kwa kutumia fimbo, mateke na ngumi.
Amedai kuwa, baada ya kuona mtoto huyo amezidiwa saa moja usiku wa Januari mosi, 2025 aliamua kumpeleka Hospitali ya llasi kwa ajili ya matibabu na baadaye Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Songwe baada ya kuzidiwa.
Hata hivyo mtoto huyo alifariki akiwa anapatiwa matibabu.
"Uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha tukio hilo ni baada ya marehemu kutorudisha chenji Sh9,000 aliyopewa na mtuhumiwa baada ya kuagizwa kununua chapati. Uchunguzi wa tukio hili bado unaendelea na pindi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani," amesema Kamanda Senga.