Baba aua mtoto sababu ya cheti cha kuzaliwa

Baba aua mtoto sababu ya cheti cha kuzaliwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
- Paul Njuguna Njoroge anadaiwa kumuua mwanawe wa pekee wa kiume baada ya kuzozana na mama ya mtoto huyo

- Njuguna alikwenda kwa nyanya ya mtoto na kusubiri hadi amelala kisha akamshambulia mvulana huyo kwa panga

- Inaaminiwa kuwa, mwanamume huyo alimuua ‘mwanawe’ huyo baada ya mama kukataa kujumuisha jina lake katika cheti cha kuzaliwa cha mtoto


Polisi mjini Murang'a wanamzuilia mwanamume mwenye umri wa miaka 25 anayedaiwa kumuua mwanawe mvulana mwenye umri wa miaka mitano kwa sababu ya cheti cha kuzaliwa cha.

Makachero walimtia mbaroni Paul Njuguna Njoroge mnamo Jumatano, Aprili 10, katika kituo cha biashara cha Mukarara.


Makachero walimtia mbaroni Paul Njuguna Njoroge (kushoto) mnamo Jumatano, Aprili 10, katika kituo cha biashara cha Mukarara. Picha: Mark Wachira/TUKO.
Njuguna, TUKO.co.ke imeng’amua alimuua Collins Waweru akiwa usingizini katika nyumba ya nyanya yake katika kijiji cha Kiharu, usiku wa Jumamosi, Aprili 6.

Akithibitisha kisa hicho, Kamanda wa Polisi Murang'a Josephat Kinyua alisema mshukiwa alizozana kwanza na shangazi ya marehemu ambaye alikuwa akimlea.

“Alikatwa mkono wake wa kushoto lakini alifanikiwa kutoroka na kupiga mayowe kuwaita majirani," Kinyua aliiambia TUKO.co.ke.

Kulingana na polisi, mshukiwa alivizia usiku na kuwashinda nguvu shangazi na nyanya ya marehemu ambaye hana uwezo mkubwa wa kuona kabla ya kumuua Collins aliyekuwa amelala.

Polisi wanasema wajirani walifika na kukuta marehemu kitandani huku mpwa wa marehemu waliyekuwa wamelala naye akiwa katika mushtuko mkubwa .

Inadaiwa mshukiwa alidai mama ya marehemu alikataa kulijumlisha jina lake katika cheti cha kuzaliwa cha mwanawe.

“Mshukiwa amekiri kutekeleza mauajai hayo na anadai mama ya marehemu alikataa kulijumuisha jina lake katika cheti cha kuzaliwa cha mtoto huyo hata ingawa yeye si baba halali ya marehemu. Evans Macharia ni baba halali na jina lake lipo katika cheti hicho


“Anasema alimlea mtoto huyo na hata ingawa walikuwa hawaishi pamoja ilikuwa ni vyema jina lake kuwa katika cheti hicho ingawa mama alikataa,” mmoja wa maafisa wa polisi ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema.

Mama ya marehemu hakuwapo wakati wa tukio hilo na alifahamishwa kuhusu kifo cha mwanawe mara baada ya kuwasili nyumbani na kupata hali ya maombolezo ilikuwa imetanda.

Kufuatia visa vingi vya mauaji na migogoro ya kinyumbani Kaunti ya Murang’a, kamanda wa polisi aliwataka wakaaji kutafuta njia za kiheshima za kusuluhisha migogo yao bila ya kuua ama kuitawanya familia.

Mshukiwa alifikishwa kortini Murang’a, Alhamisi, Aprili 11, na kushtakiwa kwa mauaji ila bado anazuiliwa huku uchunguzi ukiendelea.
 
Halafu kina masumboka wanataka kutuletea bangi ati dawa ya maumivu
Pls hii isifike kenya
 
Huyo mwanaume nae, halafu kumbe yeye sio baba mzazi,,,, yeye kwanini hapigi bao ili aitwe baba eboooo
 
Back
Top Bottom