Wakuu,
Kwanza ni vizuri ieleweke kwamba, hakuna direct contact kati ya damu ya mama na ya mtoto kwa kipindi chote mtoto awapo tumboni mwa mama yake. Hii inaondoa uwezekano wa mtoto kupata maambukizi akiwa tumboni mwa mama yake au kabla ya kuzaliwa!
Mtoto aweza kuambukizwa tu wakati wa kuzaliwa au baada ya kuzaliwa ikiwa hapatachukuliwa hatua za tahazari za kuzuia hilo!
Ieleweke kuwa ngozi ya mtoto huwa ni very delicate wakati ule wa kuzaliwa kiasi cha kuruhusu uwezekano wa kupata michubuko kwa urahisi endapo kutakuwa na msuguano kati ya hii ngozi na kuta za njia ya uzazi!
Kama njia ya uzazi haitapata vilainishi vya kutosha na ikawa ni ndogo kiasi cha kuchanika na hatimaye kutoa damu, na kama ngozi ya mtoto itakuwa na michubuko wakati wa kuzaliwa, basi mtoto anaweza kuambukizwa hiv wakati huu wa kuzaliwa!
Kama mtoto atazaliwa bila maambukizi, basi anaweza kuambukizwa na maziwa ya mama yake kama tu huyu mtoto atakuwa na michubuko kwenye utumbo wake au kwenye njia yake ya chakula wakati wa kipindi kile cha kunyonya!
Ili mtoto asiambukizwe kutokana na maziwa ya mama yake basi inabidi either anyonye maziwa ya mama yake pekee kwa muda wote wa utoto wake (muda wa kunyonya) na asipewe kitu kingine, au kama hilo haliwezekani basi atumie maziwa ya ng'ombe au artificial pekee na kamwe asichanganye na maziwa ya mama! Hii ni kwa sababu maziwa ya ng'ombe au yale artificial huwa yana kemikali ambazo zina nguvu kali inayoweza kusababisha michubuko kwenye utumbo laini wa mtoto! Hivo mtoto akipewa haya maziwa yenye kemikali yatakayosababisha michubuko kwenye utumbo wake laini halafu akanyonya maziwa ya mama yake mwenye hiv, basi kuna uwezekano wa mtoto huyu kupata maambukizi kwa kuwa utumbo wake tayari utakuwa na michubuko iliyosababishwa na maziwa haya yenye kemikali!
Hivo basi, kama mtoto amezaliwa na wazazi wenye hiv, na ili mtoto wao asipate maambukizi ya hiv basi inabidi mama yake afanye au achague kitu kimoja tu kati ya hivi viwili vifuatavo:
1. Mama amnyonyeshe mtoto wake mwenyewe kwa muda wote wa kunyonyesha bila kumpa kitu kingine au kumchanganyia maziwa yoyote yale, yawe ya ng'ombe au artificial!
2. Kama hilo la kwanza hapo juu haliwezekani, basi mtoto apewe maziwa ya ng'ombe au yale ya artificial pekee bila kuchanganya na yale ya mama yake kwa muda wote wa utoto wake (kipindi cha kunyonya)!