Baba kanumba ampiga marufuku mama kanumba kutumia jina la kanumba kwa namna yoyote ile

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Katika hali ya kushangaza, baba wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba amempiga marufuku mama mzazi wa msanii huyo, Flora Mtegoa kutumia jina la Kanumba kwa namna yoyote.


Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni baba Kanumba alisema mama Kanumba hana mamlaka ya kulitumia jina la Kanumba kwani hana uhusiano nalo.
“Mimi ndiye mwenye mamlaka na jina la Kanumba kwa sababu ni la kwangu lakini namshangaa mama Kanumba kuendelea kulitumia jina hilo hata kwa watoto wasionihusu kama mtoto wa mwanaye aliyezaliwa hivi karibuni na kuitwa Kanumba Junior.

“Anahusiana nini na hilo jina wakati huyo siyo damu yangu, yeye ana baba yake kwa nini asitumie jina lake, sitaki kabisa atumie jina langu mwanangu ameshafariki na mimi ndiye mwenye mamlaka ya kutumia hilo jina,” alisema mzee huyo.
Akilizungumzia suala hiyo, mama Kanumba alisema: Sitaki kumsikia kabisa,kama vipi aende mahakamani.”
 
dah RIP STIVIN KANUMBA. huenda watu wengine nao wakapigwa marufuku.
 
Wazazi wa kanumba sijui wakoje. Yaani wamekuwa maigizo. Yule mama yeye na pombe pamoja na mama lulu. Mzee asili ya ukorofi na maneno machafu. Vilevile mama lulu naye kumtumia mwanaye kama kitega uchumi ndiko kunamsababishia lulu matatizo ya kashfa za dushelele za wakubwa ili kukidhi mahitaji. Vilevile kaachiwa mzigo wa kumlea,ambaye ni mama kanumba. Pole Lulu,tumia kinga kwa kila tendo moja.
 

Hatariiiiiii
 
Hahahaha sasa mzee kanumba mbona kuna watu wanajiita obama tz, mi sioni ubaya loh steve umeacha mzozo
 

Hizi familia zimepata stress kali sana tangu kijana atangulie mbele ya haki...
 
Hahahaha sasa mzee kanumba mbona kuna watu wanajiita obama tz, mi sioni ubaya loh steve umeacha mzozo

Ati nayeye anaimbaga wimbo wa bwana misosi... NITOKE VIPI?
 
Hawa nao wamekuwa watu wa kutafuta umaarufu tu.

Wajinga sana hawa.
 

Hapo kwenye Red, huyu Mzee amedhihirisha alivyo kigeugeu... Unampiga mtu marufuku kutumia Jina wakati huo huo unamtaja kwa jina hilo ambalo hutaki alitumie...
 
Hapo kwenye Red, huyu Mzee amedhihirisha alivyo kigeugeu... Unampiga mtu marufuku kutumia Jina wakati huo huo unamtaja kwa jina hilo ambalo hutaki alitumie...

hahahahaa kweli wewe uko makin zaidi kusoma
 
mada hiko wazi anahosisitiza mzee ni kwamba huyo mama ana mtoto mwingine kwa baba mwingine kwa nn huyo mtoto asitumie jina la baba yake wa damu? wewe ukiwa na mtoto utakubali mkeo/mzazi mwenzio uliye naye amuite jina la bwana aliyeachana nae?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…