Baba Kanumba: Ili Wema azae, anatakiwa kulala makaburini

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Baba mzazi wa aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo , marehemu Steven Kanumba ' The Great ' , Charles Kusekwa Kanumba amefunguka kuwa ili azae , staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu anatakiwa alale juu ya kaburi .

Hayo yanakuja siku chache baada ya Wema aliyewahi kuwa mchumba wa Kanumba kudai kusumbuliwa na tatizo la kukosa uwezo wa kuzaa hivyo mzee huyo kujiongeza na kusema ni kwa sababu alitoa mimba ya mwanaye huyo.

Akizungumza na waandishi wetu , baba huyo alisema kama kweli Wema alitoa mimba ya Kanumba basi atakuwa alijilaani kwa sababu ukoo wao ukitoa mimba unaweza kufa au kujilaani (kutokupata mtoto ) hivyo anatakiwa kutambika kwa kulala juu ya kaburi la mama mkubwa wa Kanumba ambaye ni bibi wa babu wa mzee Kanumba.

Alisema sambamba na hilo, Wema atatakiwa kurithiwa na ndugu wa Kanumba (kati ya kaka au mdogo wake).

"Kwenye ukoo wetu ukitoa mimba kuna mambo mawili , moja ni kufariki dunia au ' kujikila ' ( kujilaani ) kwa kutokuzaa, pengine ndicho kilichomtokea Wema, '' alisema baba Kanumba.

KUTAMBIKA KABURINI
Mzee huyo alisema kuwa mama mkubwa huyo alishafariki dunia kwa hiyo yeye na marehemu Kanumba walipaswa kwenda kaburini kwake kufanya tambiko zito, wakiwa wamevaa mavazi maalumu ya kiasili na mikononi wameshika vibuyu, jambo ambalo lingempasa Wema kukaza moyo. Alisema kuwa wakiwa kaburini hapo, Wema alitakiwa achotewe mchanga na kushikishwa kisha kusemewa maneno ya kuomba msamaha kwa kilichotokea .

VITU VYA TAMBIKO
Alisema walitakiwa waende na maziwa , unga wa mtama na hayo mavazi maalumu kwa ajili ya tambiko hilo.

KURITHIWA NA NDUGU
Aliendelea kudadavua kwamba , kwa sasa Kanumba hayupo duniani hivyo Wema anapaswa kuchukuliwa na kaka au mdogo wake wa damu kwenda kutambika, ikiwa ni pamoja na kuzaa naye ili kufungua mlango wa kizazi, hata kama ataachika basi ataendelea kupata watoto.

MAMA MKUBWA NI NANI?
Baba Kanumba alisema mama mkubwa huyo ni bibi yake mzee Charles Kanumba ambaye katika ukoo wao alikuwa mganga wa wanawake walioshindwa kupata watoto au wenye tatizo la kizazi. Hata hivyo, baba Kanumba alimalizia kwa kusema kuwa, ingekuwa zamani ilikuwa ni kurithiwa tu lakini kwa sasa mila hizo zinapingwa vikali. Gazeti hili lilipomtafuta Wema ili kumfikishia taarifa hizo hakupatikana hivyo jitihada zinaendelea.

Chanzo: GPL

 

Attachments

  • 1431589409887.jpg
    35.7 KB · Views: 1,752
Mbona hayo ni masharti ni magumu? Aje kwetu mbegu tunazo!
 
Mambo ya mila za watu hizo, wakati mwingine huwa kweli.
 
Mama mkubwa ambaye ni bibi wa babu wa mzee Kanumba!!!!??
 
Kwa maelezo hayo Wema hana la kufanyia kazi kwa sababu mzee mwenyewe amesema hayo mambo kwa sasa hayapo.

Labda tunapata funzo kuwa kutoa mimba ni vibaya na hakuna kurithi mke wa nduguyo kwa sasa. Sioni cha ziada.
 
Mambo ya mila za watu hizo, wakati mwingine huwa kweli.

unless kumbukumbu zangu hazijakaa sawa...si alipataga mimba ya ndomo ikatoka kipindi kile walikua wanataka kuachana kwasababu ya penny cjui...ndo ilikua geresha au???? hapo mbona alipata isiyokua ya ukoo wa kanumba???
 
unless kumbukumbu zangu hazijakaa sawa...si alipataga mimba ya ndomo ikatoka kipindi kile walikua wanataka kuachana kwasababu ya penny cjui...ndo ilikua geresha au???? hapo mbona alipata isiyokua ya ukoo wa kanumba???

Sikiliza kuna baadhi ya mila huwa ninasikia kuwa ukitoa mimba ya mtu ambaye wana miiko ya kutokutoa mimba utakufa au uzazi wako utakua na matatizo.
Kama hivyo hata ukibeba mimba zinatoka na hata ukizaa mtoto atakufa.Kwahiyo itabidi ukatambikie sijui kama alivyosema baba Kanumba.
Mimi sijawahi kushuhudia hilo ila hua nasikia tu.
 
Haya sasa mambo ya kuchomoa mimba za watu hata huwajui kuna koo nyingine mimba haitoki hata iweje haya kazi kwakeeeeee
 
du, haya mambo mengine nikupiga goti tu na kuomba toba kwa mungu na hiyo mitambiko sisi wakristo tunailapa damu ya Yesu tu kazi kwishaaaa
 
mmmm,ukalale kaburini? mzee asichekeshe walonuna,kaburi na mimba wapi na wapi jamani.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…