Ebana wanajamvi inakuwaje?
Mjasiriamali, mwanasiasa, mchekeshaji na muhamasishaji nchini maarufu Baba Levo ametaja waliomsaidia wakati hana kitu.
Amesema kuna utitiri wa watu anaweza kuwashukuru kwa kumsaidia lakini atataja watano.
Watu ni wengi nilikuwa nalala sinza kwa jamaa anaitwa K Mazoba. Nilikuwa nadokoa msosi kwenye Friji hadi mke wa jamaa akamind ikawa sitonfahamu.
Nimeshawahi kulala Sinza kwa ghetto la jamaa anaitwa Sadi Yuda. Lilikuwa Ghetto la vibaka tulikuwa tunalala watu 15. Nilikuwa nalala uvunguni unakuta vibaka akipigwa huko anakuja kujificha uvunguni ninapolala huku damu zinamvuja nakutapakaa kwangu.
Anaendelea kusema ghetto lilikuwa na feni moja tu ile ya gari isiyozunguka ilikuwa inampuliza bosi tu.
Ukisema utaje list ya watu utataja list ya mamilion. Juma Kassim Kiroboto Nature alinikaribisha na kuniingiza TMK wanaume. Wakati huo inspector Haroun hawataki niingie kwenye kundi. Nature akawaambia ambae hawamtaki huyu dogo aache kundi.
Mimi njaa ilikuwa inanipiga duniani hamna mtu aliyekuwa ananisaidia kula kama Shilole Shishi food. Nilikuwa nakula hadi nikampa Jina kula jigaragaza. Tena bure pale kwake bila kutoa mia.
Hapo mbeleni nilikuwa nawabeza kuwadharau hawa kina mwijaku, baba levo na Dotto magari ila hawa jamaa wamepiti0a magumu nimetoka kuwakubali.
Pia imetokea kuwakubali sana Shilole na Juma Nature. Nature nilimchukiaga bure sana baada ya bifu na Mh. Temba ila kumbe jamaa poa sana. Nature na Shilole na wengine Mungu awabariki .
Sasa hivi Baba Levo na Mwijaku wako China wakiwakilisha vema Tanzania na kutangaza Silent Ocean Simba wa Bahari. Mungu awatangulie hawa miamba.