Baba mkubwa amenidhulumu mali zangu, nitawezaje kuzipata?

spleen

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2013
Posts
4,079
Reaction score
6,788
''Nikiwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza ndipo baba yangu kipenzi aliweza kunitoka duniani,nakumbuka tulikuwa hospitali ya taifa ambapo baba yangu alikuwa amenikumbatia huku akiwa ananiambia baadhi ya maneno"mwanangu naomba uzitumie mali nilizokuachia kwa ajili ya kusoma,mimi naenda mbali kutalii nitarudi", ndipo aliponituma nje kwenda kumnunulia tango,lakini niliorudi nilikuta ameshakufa.

Mkasa hupo hivi, viambatanishi vyote vya mali alizoniandikisha aliweza kumuachia mama yangu mzazi ambaye bado yupo hai ingawa anaumwa umwa sana.

Ndipo baba mkubwa walipokuja na shangazi wakisema wanataka wampe mama wa mtoto wa kiume mali (ikumbukwe baba alikuwa na watoto wawili, mimi wa kike na mwengine mkubwa wa kiume ambaye alifariki akiwa mafunzoni jeshini,sema kila mtoto na mama yake), bila kujua hili wala lile mama aliwapa viambatanishi vyote ndipo walipofanikiwa kubadilisha majina yote na kuweka majina yao, kiukweli inauma sana kwani waliniambia mimi sio mtoto wao na hawanijui.

Kipindi mama alipokuwa anafanya biashara tuliweza kwenda kwa mwanasheria, tulipofika mahakamani walimtafuta kijana wa kiume na kusema ni mtoto wa baba lakini ikaonekanika kwamba vyeti hafinanani na uhalisia(wametuongopea).

Nimejairibu kufanya juhudi za hapa na pale ili kusaidiwa lakini inaonekanika kila wakili ba mkubwa huwa anamnunua, kuna mzee mmoja mpaka sasa yupo Ngerengere rafiki yake na baba ndie aliyeonesha nia ya kunisaidia.

Msaada wana jamii forum,tena wa kisheria ni wapi naweza kuanzia na ushahidi gani utahutajika ili niweze kupata mali za baba,ingawa mama ananikataza lakini mi mwenyewe nahisi nina deni nahitaji kulilipa".

NOTE:
-Elimu ni kidato cha nne, kwa sasa nalima na kujishughulisha na shughuli za saluni(nimeajiliwa).
-ba mkubwa ni diwani wa katafulani morogor mjini,pia ana maduka yake na shule ya awali.
-bibi mzaa baba alionesha kunisadia mwanzoni lakini sasa yupo kimya
-mali alizoniachia baba ni nyumba mbili moja ipo mahenge, nyingine morogoro mjini, gesti house ipo morogoro mjini, magari kazaa
 
Pole sana mdogo wangu ngoja waje wataalam wa sheria watakusaidia
 
Mmh! Pole sana binti. Ngoja waje wale wanaojiita "Learned Brothers" wanasheria Bila shaka watakupa ushauri makini. Nahisi huyo mheshimiwa diwani atakuwa ni kutoka kwenye kile chama chetu ambacho self interests is more valued than community interests.
 
Nadhani TAWLAE na Legal and HUman Rights Centre wanaweza kukupatia msaada kwa gharama nafuu. Pia kuna shirika zamani likiitwa WLAC (sina haakika kama wapo very active siku hizi), ni watu wa msaada mkubwa kwa watu kama nyinyi
 
Nenda Kwa baba yako mkubwa mwambie wote tutakufa na kuziacha hizi Mali mwambie aweke hazina yake mbinguni kusiko na mchwa wala nondo.mwambie na zake zitapotea kama alizothulumu.kisha ondoka na sali sana tenda mema na ufanye kazi Kwa bidii utazidishiwa
 
nenda Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) ofisi zao zipo Ilala Boma,wanatoa msaada wa kisheria bure kwa wanawake,hapa utapoteza mda kwa kusubiri majibu ya watu,kama vipi nenda kule Jumatatu mapema watakusaidia kuliko kuanza kusubiria hapa
 
Nenda uliposhauriwa juu sababu mama yako ni mmiliki wa hizo mali as alikuwa ameoana na baba yako, na hakuweka sahini au kuruhusu mali zibadilishwe majina kuna sheria juu ya hilo la kubadili au hata kuuziwa.

Na uendelee kusali, Mungu atakufungulia. pole

Tanzania Women Lawyers Association (TAWLA).

TAWLA House,
Plot 33 Ilala Sharif Shamba
PO Box
DSM
Dar Es Salaam 9460
Tanzania [h=4]Phones:[/h] T: +255 (0) 222 862865
Welcome to TAWLA Website - TAWLA
 
Pole sana chukua namba ya simu na address kama alivyokuwekea mzurimie uwatafute hao wakusaidie, kwa vile mama umesema ni mgonjwa mgonjwa basi hili ni la kulifanya kwa haraka ili hawa wanasheria waongee naye ili awape details zaidi. Pole sana na kila la heri.
 
Last edited by a moderator:
mzurimie;

ahsante mkuu kwa kunipa info,naamini nitazifanyia kazi
 
Last edited by a moderator:
kama si wasimamiz wa mirathi..they are "executors of their own wrong"...ambalo ni kosa kisheria wanapaswa kushtakiwa na watarudisha hizo mali
 
Mtoa mada tunaomba uweke namba yako ya simu. Mimi ni mwanafunzi wa sheria chuo Kikuu mzumbe morogoro nikiwa na wenzangu tunahisi haki unayo lakini kuna baadhi ya taarifa tungependa tufahamu kwa ushauri Zaidi...ni vyema ukinitumia kwa msg...Shukran
 
''Nikiwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza ndipo baba yangu kipenzi aliweza kunitoka duniani,nakumbuka tulikuwa hospitali ya taifa ambapo baba yangu alikuwa amenikumbatia huku akiwa ananiambia baadhi ya maneno"mwanangu naomba uzitumie mali nilizokuachia kwa ajili ya kusoma,mimi naenda mbali kutalii nitarudi", ndipo aliponituma nje kwenda kumnunulia tango,lakini niliorudi nilikuta ameshakufa.

Mkasa hupo hivi, viambatanishi vyote vya mali alizoniandikisha aliweza kumuachia mama yangu mzazi ambaye bado yupo hai ingawa anaumwa umwa sana.

Ndipo baba mkubwa walipokuja na shangazi wakisema wanataka wampe mama wa mtoto wa kiume mali (ikumbukwe baba alikuwa na watoto wawili, mimi wa kike na mwengine mkubwa wa kiume ambaye alifariki akiwa mafunzoni jeshini,sema kila mtoto na mama yake), bila kujua hili wala lile mama aliwapa viambatanishi vyote ndipo walipofanikiwa kubadilisha majina yote na kuweka majina yao, kiukweli inauma sana kwani waliniambia mimi sio mtoto wao na hawanijui.

Kipindi mama alipokuwa anafanya biashara tuliweza kwenda kwa mwanasheria, tulipofika mahakamani walimtafuta kijana wa kiume na kusema ni mtoto wa baba lakini ikaonekanika kwamba vyeti hafinanani na uhalisia(wametuongopea).

Nimejairibu kufanya juhudi za hapa na pale ili kusaidiwa lakini inaonekanika kila wakili ba mkubwa huwa anamnunua, kuna mzee mmoja mpaka sasa yupo Ngerengere rafiki yake na baba ndie aliyeonesha nia ya kunisaidia.

Msaada wana jamii forum,tena wa kisheria ni wapi naweza kuanzia na ushahidi gani utahutajika ili niweze kupata mali za baba,ingawa mama ananikataza lakini mi mwenyewe nahisi nina deni nahitaji kulilipa".

NOTE:
-Elimu ni kidato cha nne, kwa sasa nalima na kujishughulisha na shughuli za saluni(nimeajiliwa).
-ba mkubwa ni diwani wa katafulani morogor mjini,pia ana maduka yake na shule ya awali.
-bibi mzaa baba alionesha kunisadia mwanzoni lakini sasa yupo kimya
-mali alizoniachia baba ni nyumba mbili moja ipo mahenge, nyingine morogoro mjini, gesti house ipo morogoro mjini, magari kazaa
Aisee, mwaka 2015 ulikuwa kidato cha nne na baba yako mkubwa alikudhulumu mali za urithi lakini hii leo wewe ni dokta bingwa unayelipwa mshahara ambao ni sawa na mishahara ya miez 5 ya mwalimu wa degree!!

Hongera sana kijana!!
 
Back
Top Bottom