Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Kabla hujaamua kupeleka mahali kwa watu hasa kwa wale wasio wa kabila lako husisha watu kwanza...
Kijana mmoja chakaramu alimpenda binti kutoka mojawapo ya makabila yanayofuga ng'ombe sana maeneo ya kanda ya ziwa. Bila kumuuliza mpenzi wake jamaa akaamua kufunga safari kwenda kijijini kwa wazazi wa binti kujitambulisha. Alipofika huko akajitambulisha na kuleta zawadi za kuku kama kianzio cha mahari...mambo yalikuwa hivi:
Mzee: Karibu kijana habari za wapi?
Kijana: Miye natoka mjini mzee na nimekuja kuleta ujumbe wangu wa kujitambulisha
Mzee: Ah kujitambulisha nini?
Kijana: Mzee mimi na binti yako tunaishi pamoja na nimekuja kuomba baraka zako ili nimuoe
Mzee: Umekuja kunini!!? kwa tahamaki mzee aliuliza.
Kijana: Kuomba baraka zako.
Mzee alikaa kimya kwa sekunde kidogo.
Mzee: Na hilo tenga la kuku?
Kijana: Mzee ni kifunga uchumba!
Mzee: Baba una wazazi wewe?
Kijana: Hapana mzee wazazi wangu walishafariki
Mzee: Una wazee huko kwenu?
Kijana: Wazee wa nini tena baba?
Mzee: Kijana umenitusi na kunitukana kwa namna za ajabu kabisa. Naomba uondoke hapa.
To cut the long story short...
Miaka 25 baadaye kijana (sasa mzee) anaishi na binti wa wote; wamezaa watoto na hawajafunga ndoa na hajaonana na baba mkwe tangu siku ile.