Baba na mwanae kutokufanana kundi la damu inasababishwa na nini?

kigosi D

Member
Joined
Sep 26, 2017
Posts
38
Reaction score
20
Baba na mwanae kutokufanana kundi la damu inasababishwa na nini? Na ni sahihi kwa watu hawa kutokufanana makundi yao?
 
Coz mtoto anayo damu yake na baba damu yake.
Kuweka mbegu kwa mwanamke ashike mimba haiend na damu zako
 
Kwa maana ya kila mtu na kundi lake pasipo mfanano sivyo?
 
Yap, na inaweza tokea yakafanana au yasifanane. Kama ilivo kwa muonekano wa mwili.

Baba anaweza kuwa mrefu kiasi ila akapata katoto kafup kidogo.
Kwa maana ya kila mtu na kundi lake pasipo mfanano sivyo?
 
Yap, na inaweza tokea yakafanana au yasifanane
Kama ilivo kwa muonekano wa mwil
Baba anaweza kuwa mrefu kiasi ila akapata katoto kafup kidogo

Hapo nimekupata vema [emoji1545]
 
Attachments

  • Screenshot_20181208-171329_1544278456067.jpg
    Screenshot_20181208-171329_1544278456067.jpg
    32.2 KB · Views: 220
Baba na mwanae kutokufanana kundi la damu inasababishwa na nini? Na ni sahihi kwa watu hawa kutokufanana makundi yao?
📌 Kwa kawaida kuna makundi makuu manne ya damu ya Binadamu. Makundi haya yanajulikana kwa majina yafuatayo:- (a) Damu group A, (b) Damu group AB, (c) Damu group B, (d) Damu group O.⁣
~ Katika makundi haya kunaweza kuwepo kwa kundi lenye Protini ya damu na kundi jingine ambalo halina protini ya Damu. Aina hii ya protini inayopatikana kwenye makundi ya damu inayojulikana kwa jina la kitaalamu kama Rhesus Factor au kwa kifupi (Rh)
~ Hivyo basi kutokana na ufahamu huu ina maana kwamba kuna mgawanyiko katika makundi makuu manne ya damu ambayo ni
(a) Kundi la Damu yenye Protini ya Resus factor.
~ Hili ni kundi la damu lenye protini ya Rhesus factor na litajulikana kama Kundi la damu la Positive. Kundi hili litatofautishwa na makundi mengine kwa alama ya kujumlisha (+) ikimaanisha kundi la damu lenye protini ya Rhesus Factor . Kwa maana hiyo kutakuwa na Group A Positive (A+), Group AB Positive (AB+), Group B Positive (B+) na Group O Positive (O+).

B. Kundi la Damu ambalo halina protini ya Rhesus factor
⁣ ~ Kundi hili la damu ambalo halina protini ya Rhesus factor litajulikana kwa jina la kundi la damu la negative. Kundi hili litatofautishwa na makundi mengine kwa alama ya kutoa (-) ikimaanisha Kundi la damu ambalo halina protini ya Rhesus Factor . Kwa maana hiyo kutakuwa pia na Group A Nestive (A-), Group AB Negative (AB-), Group B Negative (B-), na Group O Negative (O-)

KUTOWIANA KWA DAMU YA BABA NA MAMA
~ Tatizo la kutowiana kwa damu ya Baba na Mama hutokea iwapo Kundi la damu la mwanamke ambaye ni mama kuwa na Rhesus Factor Negative (-) kwa maana kwamba halina protini ya Rhesus factor na kundi la damu la mwanaume ambaye ni baba kuwa na Rhesus Factor Positive (+) kwa maana kwamba kundi lake la damu lina protini ya Rhesus factor.
~ Wanandoa hawa wanapokutana kimwili wanaweza kupata mtoto mwenye kundi la damu lenye Rhesus factor Positive (+). Na hapo hapo tukumbuke kwamba mtoto huyu mwenye Rh (+) anakwenda kuishi tumboni mwa mama yake mwenye kundi la damu ambalo ni Rh (-)
~ Tatizo hujitokeza iwapo damu ya mtoto yenye Rh positive, itakapoingiliana au kugusana kwa bahati mbaya au kuchanganyika kidogo na damu ya mama yenye Rh Negative wakati mtoto akiwa tumboni au wakati wa kujifungua.
~ Kitendo cha damu za wawili hawa yaani mama na mtoto kuingiliana kitasababisha mchakato wa kivita kwa sababu daima "HASI" (negative) na "CHAYA" (Positive) ni maadui kiasili. Vita hivi vya kimchakato vinaweza kupelekea matokeo yafuatayo:-
(a) Mtoto kufia tumboni baada ya kushambuliwa na kinga-mwili za mama baada ya kutambuliwa kama ni adui.
(b) Mtoto kufariki muda mchache baada ya kuzaliwa kutokana na kudhurika vibaya na mashambulizi ya kingamwili ya mama.
(c) Mtoto kuzaliwa akiwa na aina fulani ya ulemavu.
~ Kumbuka utafauti huu unatokana na kuwepo ama kutokuwepo kwa protini aina ya Rhesus wala sio utofauti wa kundi moja na lingine mfano A na B.⁣

Iwapo mama ambaye hana protini hizi kwenye damu mfano ana kundi A NEGATIVE akapata ujauzito kutoka kwa mwanaume mwenye protini hizi kwenye damu yake mfano baba ana kundi A POSITIVE, mtoto atarithi protini hizi kutoka kwa baba.⁣

USHAURI KWA WANANDOA.
~ Mwanamke ambaye hana protini hizi za Rhesus Factor, mfano Damu yake ni kundi A negative na ameolewa na Mwanaume mwenye protini hizi mfano kundi lake a damu ni A POSITIVE anashauriwa kuchoma sindano itakayo saidia kupunguza hatari ya kupata madhara wakati wa ujauzito.⁣

Wakati gani mama apewe hii dawa?⁣
Mama anaweza kupewa hii dawa katika hali zifuatazo:-⁣
•Wiki ya 28 ya ujauzito ⁣
•Ndani ya masaa 72 baada ya kujifungua⁣
Pia mama anaweza kupewa hii dawa iwapo ujauzito umetoka au kuharibika na wakati mwingine wowote ambao daktari ataona kuna umuhimu.⁣

By JK.
 
Well said Mkuu 🙏

Umefanya nikumbuke Biology ya form 3 🙌
 
Back
Top Bottom