EEX
JF-Expert Member
- Oct 19, 2014
- 3,781
- 12,091
Leo nimeamua kushea nanyi wanajukwaa ,hadithi fupi ya jamaa yangu Baba Peter na ningependa kwenye uzi huu atambulike kama Baba Peter.Kwa kifupi baba Peter ni mtu wa masanga/pombe/ulabu na ameshindwa kujicontrol .Lakini sisi jamaa zake hatuna tatizo ni maisha yake aliyochagua(Kwani kupanga ni kuchagua).Siku hii hasa ndio imenifanya nilete hiki kijistory.Tumetoka kwenda kwenye "party" ya jamaa yetu ,watu tumekula vizuri ,wakuonja tumeonja,Baba Peter alikunywa kama mwisho wa dunia.Basi ikafika mwisho wa kuburudika na muziki pamoja na maharusi.Kibao motomoto cha kitambaa cheupe kikapigwa.Kila mtu akatoa leso akipunga hewani tofauti ilikuwa kwa Baba Peter yeye badala ya kutoa leso akatoa mfuko wa nyuma chupi ya mama Peter huku akipunga hewani kwa madaha ,mimi binafsi nimeshikwa na butwaa .Wee Baba Peter ,we Baba Peter ilisikika sauti ya mama Peter kwa huzuni ,huku mi nikipotelea mlangoni.Jana tumekutana msibani na jamaa yangu ,punguza pombe Baba Peter.