Samandarojk
Member
- Sep 25, 2016
- 55
- 23
Kwa miaka mingi dunia ilipitia changamoto nyingi sana kwa baadhi ya jamii kuzitawala jamii nyingine au taifa moja kulitawala taifa jingine katika kila nyanja kuanzia siasa, uchumi, biashara na hata huduma za jamii. Uvamizi huo uliwafanya wazawa kutokuwa na maamuzi yeyote katika ardhi yao mama, hivyo walibaki na manung'uniko bila kuchukua maamuzi yeyote kwa kukhofia nguvu alizokuwa nazo mtawala wao, na yeyote ambaye angejitolea kupinga kinagaubaga juu ya jambo baya walilofanyiwa, kupigania mali zao au kupigania haki yao ya kupata huduma za jamii kama chakula, mavazi, malazi na huduma za afya. Basi mtu huyo yangemkuta mateso na adhabu zisizo na mifano, ni msaliti kwa mamlaka ila ni shujaa kwa jamii yake kwa kuonesha ujasiri na uthubutu wa kuikomboa jamii yake katika hali ya udhalili ili kuifanya kuwa jamii sharifu.
Wapo waliopoteza maisha katika mapambano hayo, wapo waliopoteza mali zao, wapo waliopata vilema vya maisha. Lakini masikitiko makubwa ni kuwa baada ya kufanikisha kupatikana kwa waliyokuwa wanayapigania, basi jamii huanza kwa kuwatoa thamani kutokana na udhalili waliokuwa nao na wanaenda mbali zaidi kwa kusahau fadhila zao, wanasahau kuwa hali hiyo imetokana na kujitoa kwao kwa ajili yao. Ziwapi familia za wanamajimaji? Ziwapi familia za wanamaumau? Hakuna anayetajika katika dunia ya sasa, hakuna anayefaidika na matunda ya familia zao.
Dunia kwa sasa imepiga hatua kubwa sana ya kuhama kutoka katika nyakati hizo za utumwa na kuhamia katika vita moja kubwa, vita ya uchumi, uchumi katika familia. Gharama za kuendesha familia zinaongezeka kila kukicha, mavazi ya mitindo ya kisasa, vyakula vya kileo vyenye viungo vya kila namna, maradhi nayo ni kama mifugo iliyofunguliwa asubuhi kwenda malishoni na suala la elimu nalo limetamalaki kila kona kutoka katika ngazi ya familia na jamii, na kuwa suala la dunia nzima ili mtu atambulike kama amesoma lazima awe na karatasi za kuthibitisha kauli yake zilizotoka katika taasisi inayotambulika. Vita hii inahitaji mwanajeshi imara, mwenye nia na uthubutu wa hali ya juu, hapa tunakutana na shujaa BABA.
Baba amekuwa mtumwa wa familia yake kila siku, kwa kuamka asubuhi sana (wakati mwingine bila hata ya kupata kifungua kinywa) na kurudi nyumbani nyakati za usiku ambalo ni tatizo pia kwa mpenzi wake. Siku yake huisha kwa mikimiki ya kila namna huenda asipate chochote kitu na huenda akapata kichache ambacho hakiwezi kutosheleza huduma zote katika familia yake, hivyo humlazimu kubeba deni ili kuona familia yake ikiendelea kuwa na furaha.
Kuhakikisha tabasamu linaendelea kutawala nyumbani kwake wakati mwingine baba huchukua maamuzi magumu ya kuwa mbali na wapendwa wake, hulala sehemu dhaifu, hula kisichoshibisha, huvaa kisichopendeza na hapati muda wa kupumzika.
Katika kuipambania familia yake baba anakuwa hana muda mwingi wa kukaa na familia yake, hapati nafasi ya kupiga soga na watoto wake, kwake ni kutoa huduma inayotakiwa na kukemea jambo baya linalofanywa. Hivyo watoto wengi humuona baba kama si rafiki, hana upendo wa dhati, hawasikilizi, mtu mkali anayetoa amri tu
Kutokana na hayo hupunguza upendo kwake wakiwa katika umri mdogo hukua katika namna hiyo mpaka wanapokuwa na umri mkubwa, ambapo baba hana nguvu tena za kupambania familia wala kujipambania mwenyewe akiwa na matarajio makubwa kupata msaada kwa watoto wake ambao aliwapigania wakiwa wadogo. Na ndipo wakati huo watoto humpa kisogo, wakidai kuwa hakuwa karibu nao walipokuwa wakimuhitaji sana. Wanasahau kuwa yeye ndiye shujaa wao ambaye amepigania makuzi yao, amehakikisha afya yao, amehakikisha malazi yao na malaji yao, amewapa heshima mtaani kwa elimu yao.
Fauka ya hayo jamii inapaswa kubadilika na kumuenzi shujaa huyu ambaye anayejitoa kwa hali na mali kuhakikisha jamii inakuwa sehemu salama na yenye amani, pamoja na mapungufu yake yote lakini yote hayo yanatoka na harakati zake katika kuleta tabasamu katika familia yake.
Baba ni shujaa! Baba ni rafiki! Baba ni mlezi!
Heshima kwa kina baba wote.
Mungu wabariki baba zetu.
Ameen.

Upvote
1