chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,969
Baba wa muimbaji wa ‘Burger Movie Selfie’, Belle 9 amefunguka kuwa hapo mwanzo hakutaka mwanae afanye muziki na badala yake alipenda aingie kwenye kilimo.
Amesema mwanae alipomaliza tu darasa la saba, alitaka alishike jembe.
Mama wa Belle 9 akiwa na mtangazaji wa Clouds, Casto Dickson
Akiongea kwenye kipindi cha Siz Kitaa kinachoruka kupitia Clouds TV, Baba wa Belle 9 amedai kuwa sababu iliyomfanya asitake mtoto wake huyo aingie kwenye muziki ni kutokana na kuogopa angejihusisha na vikundi vingine vibaya ambavyo vingemuharibu kama hapo zamani wazazi wengi walivyokuwa wakifikiria na sababu kubwa ikiwa familia yao haikuwahi kuwa na msanii hata mmoja.
Pia Mzee huyo ameutaja wimbo wa muimbaji huyo ambao anaukubali kwa kusema, “Naupenda ule wimbo unaosema wazazi wangu watakukataa. Baada ya kutoka wimbo ule hata mimi nikaanza kupunguza makofi kidogo.”
Mzazi huyo amemaanisha wimbo wa mwanae anaoukubali ni ‘Sumu Ya Penzi’.
chanzo; bongo5