Baba wa Xi Jinping alimfundisha kitu gani?

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215


Mwaka 2001, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Fujian Xi Jinping alimwandikia baba yake barua ya pongezi ya siku ya kuzaliwa, akisema anatumai kujifunza sifa bora kutoka kwa baba yake.
Bw. Xi Zhongxun alikuwa mfanyakazi mwanamapinduzihodari, licha ya mambo yake ya mapinduzi pia alipenda sana kuwa pamoja na familia yake. Aliwapenda watoto wake, lakini pia alikuwa mkali sana.

Mwezi Agosti mwaka 1978, Bw. Xi Zhongxun alifanya ziara ya ukaguzi katika kijiji cha Huiyang, mkoani Guangdong. Bw. Xi Jinping ambaye alikuwa anasoma katika chuo kikuu cha Qinghua alikwenda pamoja na baba yake kwa mapumziko ya majira ya joto.

Mwaka 1978 Bw. Xi Zhongxun alipokwenda Guangdong, alichapa kazi usiku na mchana. Ili kujua vizuri zaidi hali ya mkoa huo, alitembelea wilaya 23 katika majira ya joto ya mwaka huo.
Rais Xi Jinping amerithi sifa ya baba yake ya kufanya kazi za utawala kwa bidii. Katika wilaya ya Zhengding, alifanya ziara za ukaguzi katika vijiji vyote. Alipokuwa mji wa Ningde, alikagua wilaya 9 kwa muda wa miezi mitatu. Katika mkoa wa Zhejiang, alitembelea miji na wilaya yote 90 kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja.


Mwezi Agosti mwaka 1978 Bw. Xi Zhongxun alifanya ukaguzi katika wilaya ya Boluo, mkoani Guangdong.
Mwaka 2001, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Fujian Bw. Xi Jinping alishindwa kuhudhuria sherehe ya siku ya kuzaliwa ya baba yake. Alimwandikia baba yake barua ya pongezi. Bw. Xi Zhongxun alisoma barua hiyo, na kusema kuhudumia wananchi ni upendo mkubwa zaidi kwa baba na mama.
 
Leta dili za kufanya na wachina sio historia za madikteta....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…