Maisha ni hadithi ndefu sana, Kuna wakati unaweza usiyaelewe vizuri.
Baba yako hana tofauti na baba yangu, Ila Mimi baba hakuacha kazi yeye amefanya kazi mpaka anastaafu, kwa kweli Kama ni masuala ya mali sijui uwekezaji yeye hayakumsumbua kichwa kabisa, zaidi yeye ni mtu wa kuhakikisha mezani chakula kipo na vinywaji pia.
Kiukweli yeye ana amani ya kutosha na kwa miaka 35 yote aliyofanya kazi serikalini amewahi kuuguwa na kulazwa mara moja tu, nini nataka kusema unaweza kuwa tajiri wa mali ukawa maskini wa afya, hivyo basi maisha ni yako mwenyewe yaani kuishi ulivyopanga wewe na sio wanavyopanga watu wengine.