Babati, Manyara: Ajinyonga baada ya kumuua mkewe kwa wivu wa mapenzi

Babati, Manyara: Ajinyonga baada ya kumuua mkewe kwa wivu wa mapenzi

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Babati. Mkazi wa mtaa wa Kiongozi Mjini Babati mkoani Manyara, Lucas Mangu (46) amefariki dunia kwa kujinyonga mara baada ya kumuua mke wake Anna Kisino (41) kwa kumpiga kutokana na wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Marrison Mwakyoma akizungumza na Mwananchi Digital leo Agosti 23, 2021 amesema tukio hilo limetokea jana usiku.

Kamanda Mwakyoma amesema Mangu alimuua mkewe kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili hadi kumuua baada ya kumfungia ndani kutokana na wivu wa kimapenzi.

Amesema Mangu alikuwa amesafiri kwenda Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro kwa ajili ya shughuli za kilimo na alirudi Babati siku hiyo na kufanya mauaji hayo ya mkewe na kujiua.

“Siku hiyo baada ya kurudi nyumbani ghafla bila taarifa alimkosa nyumbani mke wake ambaye alitoka kidogo na aliporudi akamuuliza alikuwa wapi na kuanza kumpiga,” amesema Kamanda Mwakyoma.

Amesema watu walijaribu kumwambia aache kumpiga mkewe baada ya kusikia yowe ila kwa kuwa alifunga mlango akimpiga aliwaambia wamuache ampige kwani ni mkewe.

“Alimpiga hadi kumuua akajaribu kumwamsha ikashindikana akadhani ni utani alipobaini amefanya mauaji akachukua mgorori akajiua kwa kujinyonga,” amesema Kamanda Mwakyoma

Chanzo: Mwananchi

ajiyonga-pc-data.jpg

(Picha siyo halisi)
 
Tafata kamba aliyo tumia kwa mambo yangu binafsi
 
Vijana sasa wanaogopa kuoa! Maana kila siku: "Kauwa, kajiuwa". Ni bora kuwa single uishi walau maisha marefu. 41 & 46 years?
 
Back
Top Bottom