Babati, Manyara: Amuua jirani yake aliyemtuhumu kuwa anamloga

Babati, Manyara: Amuua jirani yake aliyemtuhumu kuwa anamloga

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mkazi wa Kijiji cha Mutuka Wilayani Babati Mkoani Manyara, Samson Daudi (26) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua Peter Buu (48) akimhusisha na imani za kishirikina.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Grafton Mushi amesema leo Septemba 7, 2021 kuwa tukio hilo limetokea juzi kwenye kijiji hicho baada ya Daudi kumtuhumu Buu anamloga ili nyumba yake isimalizike kujengwa.

Mushi amesema mtuhumiwa alimuua Buu kwa kumkata mara tatu shingoni kwa kutumia panga na kisha akafariki dunia papo hapo.

"Mtuhumiwa alikuwa anamtuhumu kufanya ushirikina na kukwamisha ujenzi wa nyumba yake ambayo imeshindikana kukamilika," amesema Mushi.

Amesema kabla ya tukio hilo marehemu alifika shambani mwa mtuhumiwa aliyekuwa akimtuhumu kukwamisha ujenzi wa nyumba yake kwa kumroga na ndipo ugomvi uliibuka na Daudi akaanza kumwambia kuwa anamuroga ili asimalize nyumba yake ndipo akaanza kumshambulia kwa mapanga.

Mushi amewataka wananchi kutafuta suluhu ya matatizo yao kwa kufikiria njia sahihi na siyo kwenda kwa waganga wa kienyeji ambao watawapotosha.

"Nawaonya wananchi wanaoamini kishirikina kuacha mara moja ili kuepuka kufanya uharifu wa mauaji kama haya," amesema Mushi.

Amesema mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi unaendelea muda wowote atafikishwa mahakamani pindi ukikamilika.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mutuka, Peter Yambi amesema matukio ya aina hiyo ya mauaji yalikuwa yanatokea miaka ya nyuma.
Amesema chanzo cha matukio ya namna hiyo ni vijana kunywa pombe na kutumia dawa za kulevya ambazo husababisha matukio ya kikatili.

Yambi amesema mtuhumiwa siyo mtu wa kudumu katika kijiji hicho kwa kuwa hutoka na kurudi hivyo ni vigumu kumjua vizuri tabia yake.
 
Bongo watu wanaamini sana uchawi. Utashangaa mtu na heshima zake anazungumza habari za mamba wa kutumwa, simba wa kutumwa, karogwa ili aumwe, mara karogwa ili biashara iyumbe. Mara habari za chuma ulete.

Wenzetu waliamini hayo enzi za giza na waliuana sana na kuchomana moto, baadaye akili zikawajia. Leo wanashangaa ujinga uliokuwepo medieval times. Sasa tunafanya hayo karne ya 21.

Huwa nachoka kabisa jinsi tulivyo washirikina.
 
Bongo watu wanaamini sana uchawi. Utashangaa mtu na heshima zake anazungumza habari za mamba wa kutumwa, simba wa kutumwa, karogwa ili aumwe, mara karogwa ili biashara iyumbe. Mara habari za chuma ulete. Wenzetu waliamini hayo enzi za giza na waliuana sana na kuchomana moto, baadaye akili zikawajia. Leo wanashangaa ujinga uliokuwepo medieval times. Sasa tunafanya hayo karne ya 21.

Huwa nachoka kabisa jinsi tulivyo washirikina.
Ni ngumu sana kuwatenganisha waTz na mambo ya kichawi.

Badala ya kutafakari na kutafuta sababu halisi za mikwamo yao, wanakimbilia kupiga ramli.

Mtu mvivu, anaendekeza tu umalaya na ulevi... maisha yakimpiga anatafuta visingizio.
 
Uvivu, wivu, elimu ya kubabaisha na kutaka upandishwe cheo, kutaka makuu zaidi ya uwezo wako, Bosi wako akupende nk, ni chanzo kikuu cha mambo hayo machafu.
 
Bongo watu wanaamini sana uchawi. Utashangaa mtu na heshima zake anazungumza habari za mamba wa kutumwa, simba wa kutumwa, karogwa ili aumwe, mara karogwa ili biashara iyumbe. Mara habari za chuma ulete.

Wenzetu waliamini hayo enzi za giza na waliuana sana na kuchomana moto, baadaye akili zikawajia. Leo wanashangaa ujinga uliokuwepo medieval times. Sasa tunafanya hayo karne ya 21.

Huwa nachoka kabisa jinsi tulivyo washirikina.

..... wabongo ushirikina ni biashara, yaani wana lana
 
Ni ngumu sana kuwatenganisha waTz na mambo ya kichawi.

Badala ya kutafakari na kutafuta sababu halisi za mikwamo yao, wanakimbilia kupiga ramli.

Mtu mvivu, anaendekeza tu umalaya na ulevi... maisha yakimpiga anatafuta visingizio.
Hayo mambo ni kule kwenu tu tanganyika ndio yametaradadi
 
Bongo watu wanaamini sana uchawi. Utashangaa mtu na heshima zake anazungumza habari za mamba wa kutumwa, simba wa kutumwa, karogwa ili aumwe, mara karogwa ili biashara iyumbe. Mara habari za chuma ulete.

Wenzetu waliamini hayo enzi za giza na waliuana sana na kuchomana moto, baadaye akili zikawajia. Leo wanashangaa ujinga uliokuwepo medieval times. Sasa tunafanya hayo karne ya 21.

Huwa nachoka kabisa jinsi tulivyo washirikina.
Nilifanya field katika kata fulani ipo Mbeya. Wanafunzi wakawa wanapandisha mashetani na kuwehuka kila ikifika usiku.

Kikaitishwa kikao ambapo katika hicho kikao ilikua ni kuwaambia wazee wa hicho kijiji waache hizo tabia kwakua serikali imepeleka pale huduma na wanachofanya ni kuiambia serikali kwamba hawataki huduma za kukiendeleza kijiji chao.

Baada ya madongo na wazee kusema itakua wenzao wa upande mwingine ikaamriwa kwamba basi kama ni hivyo wawaambie wenzao waache hiyo tabia na kama kuna mzee mwingine hajafika hapo naye apate taarifa. Likijirudia tukio la hivyo shule itavunjwa, na hakuna mradi utaenda pale.

Tangu siku hiyo mpaka naondoka halikutokea tena tukio la wanafunzi kuwehuka na kupandisha mashetani.
 
Back
Top Bottom