𝗕𝗔𝗕π—₯𝗔 :π—ͺ𝗔𝗧𝗨 π—ͺπ—”π— π—˜π—Ÿπ—œπ—£π—ͺ𝗔 π—£π—˜π—¦π—” π—žπ—¨π—§π—˜π—‘π—šπ—˜π—‘π—˜π—­π—” 𝗣π—₯π—’π—£π—”π—šπ—”π—‘π——π—”.

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
458
Reaction score
1,280
... πŸ—£οΈ 𝗕𝗔𝗕π—₯𝗔 - π—ͺ𝗔𝗧𝗨 π—ͺπ—”π— π—˜π—Ÿπ—œπ—£π—ͺ𝗔 π—£π—˜π—¦π—” π—žπ—¨π—§π—˜π—‘π—šπ—˜π—‘π—˜π—­π—” 𝗣π—₯π—’π—£π—”π—šπ—”π—‘π——π—”.

"Propaganda zilizofadhiliwa zimefikia hatua ya kuchukiza sana kama vita za kisiasa. Kwani hatuwezi kuona kikamilifu nyuma ya hii Content rahisi iliyolipiwa ?! "

©️ Barbara Gonzalez
CEO wa zamani wa Simba SC Via X

Hakuna mchakato wowote wa Barbra Gonzalez kurejea Simba kama CEO wala Mwenyekiti wa Bodi, ni kitu ambacho hakifikirii kwasasa na hakipo kwenye akili yake, taarifa kutoka kwenye vyanzo vyangu ni kuwa ukurasa wake ndani ya mpira wa Tanzania ameshaufunga.

Nachokifahamu mpaka sasa ni kamchezo kanaendelea cha kubadili upepo tena katika wakati ambao ni muhimu sana wa klabu kujiunda na kuanza upya, bahati mbaya sana propaganda zimetawala sana kuliko uhalisia, kwa ground vitu viko hovyo tu na mambo hayaendi, bahati mbaya Mashabiki washahamishiwa mjadala na wanajadili kitu kipya ambacho hakipo.

Hii klabu inatakiwa kurejesha ufalme wake ila mpaka sasa Simba kuna vitu havipo sawa halafu ni kama tunazidi kujivuruga tu, kuna Mtu ametulia sehemu anapiga mziki na anafurahi kuona Watu wanacheza, ila huu ni msiba tena unafana sana kwakuwa hakuna Mtu anayelia nje ya key, this is a very calculated move.

Wakati mchakato wa Mabadiliko umekwama na hatujui lini utaendelea inatangazwa nafasi ya Mkurugenzi wa Mashabiki na Wanachama, kwa muundo gani ndani ya Simba ambayo haidahili Wanachama wapya? Anaenda kufanya kazi gani? Anakusanya Wanachama gani? Hapo tujiulize sote kisha majibu bakini nayo.

SIMBA SC KUNA SHIDA KUBWA NA WASIPOANGALIA YANGA ANAENDA KUTAWALA MISIMU MINGINE 3 MFULULIZO.
 

Attachments

  • 1717824349786.jpg
    224 KB · Views: 3
Sawa. Basi ungempa credit FARHAN KIHAMU kwamba ume kopi andiko lake
 
Yani jamaa ame kopi Sehemu mbili halafu zote kaunganisha kiasi kwamba ukisoma kuelewa inakuwa ngumu.
 
Simba ajitahidi msimu ujao arejee nafasi ya pili
 
Simba mnajitekenya😭😭😭
 
Tutaendelea kumsubiria Barbara aje hata kama itakuwa ni miaka 1000 ijayo! 🀣🀣🀣🀣🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…