“Wewe ndiye unayekwenda kupiga kura, wewe ndiye unayesema siitaki CCM, ni wewe. Sasa nyinyi mumeachiwa mitaa miwili, itakuwa miujiza mitaa hii msishinde, itakuwa miujiza kura muzipoteze, itakuwa miujiza msiende kupiga kura, kwa maana miaka 5 migumu itakuja tena. Kwa hivyo mimi ninachoweza kuwaambia kapigeni kura."
Mwenyekiti mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Juma Duni Haji maarufu kama Babu Duni akiwanadi wagombea wa chama hicho wa mitaa ya Mwinyimkuu na Idrisa katika mkutano uliofanyika Mtaa wa Mwinyimkuu Kata ya Mzimuni Jimbo la Kinondoni Novemba 22, 2024.
"Mimi ninasema mnadharau kwasababu mmekata tamaa, mnahisi mambo ni yaleyale...aah! ndiyo hivyo bana, CCM watachukua kwa nguvu; hawezi kuchukua kwa nguvu, wakichukua kwa nguvu maana yake mmewaachia, vijana mjiandae, mkipiga kura, mkishinda kataeni kunyang'anywa"- Babu Duni.