Babu Seya atahadharishwa kujiepusha na kiki

Babu Seya atahadharishwa kujiepusha na kiki

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
BABU SEYA.jpg

Mkali wa muziki wa Chakacha na Mduara AT ambaye jana tu ameachia wimbo wake mpya wa 'Kazi yao', ametoa ushauri mzito kwa Babu Seya akimtahadharisha kuhusu kiki.

Ikiwa ni muda mfupi tu tangu atoke jela, AT anamwambia Babu Seya awe makini sana na watu wanaomzunguka, wanapomshauri juu ya Kiki na matumizi ya mitandao ya kijamii.

Akipiga Stori na eNEWZ, AT amesema kuna watu wengi ambao watakuwa hawapendi kumuona Babu Seya na mwanae wakifanikiwa katika maisha jambo ambalo linaweza kupelekea wao kushindwa kutumia vizuri mitandao ya kijamii hasa katika kuhakikisha wanasapoti kazi zao.

Hata hivyo AT amesema kwamba yeye alipata shida sana haswa pale alipoanza kusikiliza maneno na ushauri wa mashabiki hali iliyopelekea mpaka akabadilisha aina ya mziki ambao alikuwa anaufanya na kuhamia katika Bongo fleva kitu ambacho anaamini kwamba kilimrudisha nyuma kisanaa.

Kwa upande wa mziki wake AT amesema ameamua kujikita rasmi katika mziki wa mduara mpaka ahakikishe anarudisha heshima ya jina lake ambalo anaona linapotea na kipindi hiki hatosikiliza ushauri wa mtu yeyote ambaye atamshauri kinyume na mipango yake.

Chanzo: EATV
 
Ulishuhudia huo ubakaji? una uhakika gani kuwa hawakusingiziwa? Kama hukushuhudia kwa macho na masikio yako huna haki ya kuwatuhumu hivo.
Kumbuka si kila aliye jela ametenda kosa alilotuhumiwa kutenda.

Na wewe acha uzwazwa. Unataka ushahidi humu JF?
 
Ulishuhudia huo ubakaji? una uhakika gani kuwa hawakusingiziwa? Kama hukushuhudia kwa macho na masikio yako huna haki ya kuwatuhumu hivo.
Kumbuka si kila aliye jela ametenda kosa alilotuhumiwa kutenda.
Ushahidi ulishatolewa mahakamani na wakakutwa na hatia...!! Wakakata rufaa na kesi ikasonga toka mahakama kuu hadi mahakama ya rufaa. Kote wakakutwa na hatia ya kubaka vitoto vidogo!

Una lingine?
 
Ushahidi ulishatolewa mahakamani na wakakutwa na hatia...!! Wakakata rufaa na kesi ikasonga toka mahakama kuu hadi mahakama ya rufaa. Kote wakakutwa na hatia ya kubaka vitoto vidogo!

Una lingine?
Kesi ilikuwa ya upande mmoja ndio maana magu kawatoa na kuwapa studio
 
Hawa ni paedophiles, hata Magufuli awapige denda hadharani, hiyo haiwezi kubadilisha ukweli.
 
Ulishuhudia huo ubakaji? una uhakika gani kuwa hawakusingiziwa? Kama hukushuhudia kwa macho na masikio yako huna haki ya kuwatuhumu hivo.
Kumbuka si kila aliye jela ametenda kosa alilotuhumiwa kutenda.
Watu wa aina yako ni hatari kwa usalama w watoto. Unapikuwa upande wa waovu unajivisha uovu. Mwnwndo wa kesi unaonyesha watoto tisa walinajisiwa na watoto hao walitoa ushahidi na baadhi waliokuwa na majeraha walithibitishiwa na daktari kufanyiwa vitendo vya unajisi.
 
Ulishuhudia huo ubakaji? una uhakika gani kuwa hawakusingiziwa? Kama hukushuhudia kwa macho na masikio yako huna haki ya kuwatuhumu hivo.
Kumbuka si kila aliye jela ametenda kosa alilotuhumiwa kutenda.
Mwenye hadidu za rejea za kesi na hukumu ya babu seya atusaidie kama Tanzania kuna wandishi watusaidie ikiwa ni pamoja na kumuhoji akimu aliyesimamia hiyo kesi na victim
 
Wakumbushwe kuwa jamii bado inawatambua kama wabakaji
 
Back
Top Bottom