Babu wa Loliondo anaswa Benki....

Boflo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
4,383
Reaction score
4,412






Stori:Mwandishi Wetu
Katika kuonesha kuwa Mchungaji Mstaafu, Ambilikile Mwasapile ‘Babu wa Loliondo' bado ana fedha baada ya kuzikusanya kutoka kwa wateja wake wa huduma ya kikombe, hivi karibuni alinaswa ndani ya Benki ya NMB akipata huduma.


Babu alibambwa ndani ya benki hiyo Tawi la Loliondo mkoani Manyara akihudumiwa na mmoja wa wafanyakazi aliyefahamika kwa jina la Lembris Lesion ambapo inaelezwa alikuwa akielekezwa jinsi ya kujiunga na huduma mpya ya Jisevie.
Akiwa benki hapo, Babu alionekana akijaza fomu huku akiwa na begi ambalo linashukiwa kuwa na fedha ndani yake ambapo baadhi ya watu waliokuwa wakimpiga chabo hawakuonesha kumshangaa wakiamini bado ana mkwanja wa kutosha kutokana na ile tiba ailiyokuwa akiitoa kwa watu wengi hivi karibuni.
"Unajua Babu alipata pesa nyingi sana na bado anaendelea kuzikusanya, kimsingi ana pesa ndefu benki," alisema mmoja wa wateja aliyekuwa eneo hilo. GPL
 
Hahahahhaha watu wabaya kwa kufuatilia,babu ni celebrity zaidi ya wazee wa bongo movie na mjengo wake sasa uko poa tu ila hakika babu angekuwa mtasha basi lazima wangemuingiza kwenye lile tabu lao ka kumbukumbu kwa kuwa mtu aliyekusanya umati mkubwa wa watu kwa pamoja na kusababisha foleni ya magari zaidi ya 20 km
 
Wakuu, Hapo babu kafanya la maana sana kuzipeleka fedha Benki, Bora zitazunguka na kuleta manufaa
kwa uchumi (circulation) kuliko kuzichimbia.
akatuletee zingine!!
 
biashara ya miamia, miambili, tano na buku ndo mpango mzima wa maendeleo, alitakiwa afungiwe EFD ili kujua mapato alopata
 
Entrepreneurship at old age, nice!
Ila babu ametisha. Wakati akina Albert Einstein walijulikana kwa kugundua mabomu ya nyuklia, babu maarufu kwa dawa ya kikombe ambayo in Tsh. 500 (0.3USD).
It only takes the mind to impact, not gold and silver
 
Huyu ni wakushtakiwa na kufungwa kabisa amewaibia watu sana
 
Economic explanation mkuu!
yaani big amount aliyocollect na akazidepositi na mie na wewe tukapatepo kamkopo for small scale investmnts au
ujasirimal kuwainua wafanyabiashara na wengi kunyanyua kiwango. Mabenki yatachangia kuboresha na kujenga taifa.
 
babu alivyoanza kutoa huduma baada ya miez michache askofu wa kkt arusha alisema kias walichokusanya ni BILLION 1.5 na hiyo ilikuwa zaman,kibongo bongo BABU inafaa aingizwe kwenye list ya FORBES
 
Acha anenepe, kwakuwa watu walienda kwa hiyari kupata kikombe kuliko kuwa jangili. Kinana tasker lager hoyeeeeeeeeeeeeee
 
wabongo bwana ona babu shavu nono waliofiwa na ndugu zao sijui wanajiskiaje kwa sasa duuuuuuuuuuuu:first:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…