Baby Diapers bussiness

Kipengeleto

Member
Joined
Feb 21, 2024
Posts
47
Reaction score
90
Habari wana jamvi wenzangu.

Baada ya kuona jambo hili na kuliangalia jinsi linavyoenda nimeona nilete kwenu kwa msaada wa zaidi. Nahitaji kwa mwemye uzoefu na biashara hii anisaidie mambo haya katika biashara ya dipers/ maarufu kama Pampers.

1. Supplier/ msambazaji wake mkuu ambae anauza bei za jumla

2. Bei zake. Na je zina faida kiasi gani. Mfano kama naanza na mtaji wa mil. 2

3. Sina shaka na marketing issue maana kila napopita naona zinaweza uzika bila tatizo ( watoto ni wengi).

4. Yapi mabaya na hasara nazoweza pata katika mchakato huu?

5. Brand zipi zina soko sana na zinapendwa kutokana na unafuu wa bei na ubora wa bidhaa hiyo?

Tafadhali kwa mwenye ujuzi na biashara hii atumwagie data hapa.

Nawakilisha kwenu wadau.
 
Huwez kuwa supplier kwa 2M,
Kisha faida ipo ya kawaida,
Zinazotoka sana ni babycheeky


Kama una mtaji mkubwa fanya ila mtaji mkubwa sio 2M
 
Huwez kuwa supplier kwa 2M,
Kisha faida ipo ya kawaida,
Zinazotoka sana ni babycheeky


Kama una mtaji mkubwa fanya ila mtaji mkubwa sio 2M
Tupe information
 
Ukiweza kupata diapers zenye ubora kama wa Sleepy utakuwa umemaliza kila kitu maana zile zinakaa siku nzima kama mtoto hakati gogo zaidi ya mara moja kwa siku aaah unakuta kwa siku umetumia mbili tu moja atashinda nayo moja akiwa anaenda kulala usiku.
 
Ukiweza kupata diapers zenye ubora kama wa Sleepy utakuwa umemaliza kila kitu maana zile zinakaa siku nzima kama mtoto hakati gogo kila siku aaah unakuta kwa siku umetumia mbili tu.
Asanteee mkuu,nitazitafuta.
 
Ukiweza kupata diapers zenye ubora kama wa Sleepy utakuwa umemaliza kila kitu maana zile zinakaa siku nzima kama mtoto hakati gogo kila siku aaah unakuta kwa siku umetumia mbili tu.

Sleepy ni nzuri mnoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…