Baby Madaha: Natamani Zitto Kabwe anioe, ni mwanaume jasiri

Baby Madaha: Natamani Zitto Kabwe anioe, ni mwanaume jasiri

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2014
Posts
9,866
Reaction score
5,747

attachment.php

Nyota wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha


Gladness Mallya
NYOTA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha amesema kuwa anatamani kuolewa na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Zuber Kabwe, akisema ni mwanaume mwenye sifa zote za kuwa mume kwa mwanamke anayejiamini, Risasi Mchanganyiko linakupa full mkanda.

Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, Baby Madaha ambaye alizungumzia masuala mbalimbali ya sanaa na kijamii, alisema Zitto ni mwanasiasa anayejiamini anayejua kusimamia hoja zake, hivyo kumpata mtu wa namna hiyo, ni kitu anachokitamani kitokee.

"Nafikiri Zitto ni mwanaume anayenivutia sana ambaye ningetamani anioe, licha ya kujiamini kwake, pia ana akili na ujasiri wa hali ya juu, kitu ambacho wengi hawana. Ukiangalia mambo ambayo ameyafanya akiwa bungeni, yanaonyesha ni jinsi gani yeye ni mtu jasiri ambaye yupo tayari kufa kwa kupigania anachokiamini," alisema Baby.

Kuonyesha kuwa anamfuatilia mwanasiasa huyo kijana, aliorodhesha mambo kadhaa yaliyosimamiwa na Zitto bungeni bila kuogopa, la mwisho kabisa likiwa ni sakata la upotevu wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, ambalo liliishia kwa wanasiasa kadhaa kupoteza nyadhifa zao, akiwemo aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliyekuwa Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi.

Licha ya kumpenda Zitto, Baby Madaha pia alisema anahusudu kujiunga na jamii ya Freemason, akisema anavutiwa na jinsi wanavyojitoa katika kusaidia watu wa jamii mbalimbali, tofauti na imani ya wengi kuwa watu hao ni wabaya.

Alitoa kauli hiyo kufuatia swali lililomuuliza imani yake kwa mambo ya kishirikina, tabia inayosemwa kufanywa na baadhi ya waigizaji na wanamuziki hapa nchini.

"Ukiniambia Freemason kweli, uchawi? Napenda Freemason maana iko wazi na kiongozi wake anajulikana, tofauti na imani za giza ambazo wahusika hawaonekani, achilia mbali kuwa wengi wao ni wachafu na wenye maisha ya shida.

"Muangalie mtu kama Chande (Alex, Kiongozi wa Freemason Tanzania) ni mtu mwenye maisha mazuri na yupo watu wanamuona, anaendesha taasisi kwa uwazi, haijalishi wako vipi, mimi ninawaelewa na ninawakubali," alisema msanii huyo na alipoulizwa kuhusu usiri wa baadhi ya masharti ya kujiunga kama yana ishara mbaya, aliongeza;

"Siyo kila kitu mtu ajue, lazima yawepo baadhi ya mambo mnayojua wenyewe tu, angalia hata shoo ya Diamond, ameweka kiingilio kikubwa kwa sababu siyo kila mtu lazima aingie, wengine wa oyaoya waishie hukuhuku, huko kuna wenyewe, binafsi nitafurahi sana nikipata chansi, hao waliomo humo mbona hatuoni watoto wao wamekufa au wazazi wao?," alisema kwa kuhoji Baby.


CHANZO: GPL
 

Attachments

  • madaha.jpg
    madaha.jpg
    30.5 KB · Views: 2,279
Akizungumza katika mahojiano maalum na
gazeti hili wiki iliyopita jijini Dar es Salaam,
Baby Madaha ambaye alizungumzia masuala
mbalimbali ya sanaa na kijamii , alisema Zitto
ni mwanasiasa anayejiamini anayejua
kusimamia hoja zake , hivyo kumpata mtu wa
namna hiyo , ni kitu anachokitamani kitokee .
Mh . Zitto Zuberi Kabwe
“Nafikiri Zitto ni mwanaume anayenivutia
sana ambaye ningetamani anioe, licha ya
kujiamini kwake, pia ana akili na ujasiri wa
hali ya juu, kitu ambacho wengi hawana.
Ukiangalia mambo ambayo ameyafanya
akiwa bungeni, yanaonyesha ni jinsi gani yeye
ni mtu jasiri ambaye yupo tayari kufa kwa
kupigania anachokiamini , ” alisema Baby .
Kuonyesha kuwa anamfuatilia mwanasiasa
huyo kijana , aliorodhesha mambo kadhaa
yaliyosimamiwa na Zitto bungeni bila
kuogopa, la mwisho kabisa likiwa ni sakata la
upotevu wa fedha katika akaunti ya Tegeta
Escrow, ambalo liliishia kwa wanasiasa
kadhaa kupoteza nyadhifa zao, akiwemo
aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini ,
Profesa Sospeter Muhongo, aliyekuwa Waziri
wa Nyumba , Ardhi na Maendeleo ya Makazi,
Profesa Anna Tibaijuka , Mwanasheria Mkuu
wa Serikali , Fredrick Werema na Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini , Eliakim
Maswi .
Licha ya kumpenda Zitto , Baby Madaha pia
alisema anahusudu kujiunga na jamii ya
Freemason , akisema anavutiwa na jinsi
wanavyojitoa katika kusaidia watu wa jamii
mbalimbali , tofauti na imani ya wengi kuwa
watu hao ni wabaya .
Alitoa kauli hiyo kufuatia swali lililomuuliza
imani yake kwa mambo ya kishirikina , tabia
inayosemwa kufanywa na baadhi ya waigizaji
na wanamuziki hapa nchini .
“Ukiniambia Freemason kweli , uchawi ?
Napenda Freemason maana iko wazi na
kiongozi wake anajulikana, tofauti na imani
za giza ambazo wahusika hawaonekani ,
achilia mbali kuwa wengi wao ni wachafu na
wenye maisha ya shida.
“Muangalie mtu kama Chande ( Alex , Kiongozi
wa Freemason Tanzania ) ni mtu mwenye
maisha mazuri na yupo watu wanamuona ,
anaendesha taasisi kwa uwazi , haijalishi
wako vipi , mimi ninawaelewa na
ninawakubali , ” alisema msanii huyo na
alipoulizwa kuhusu usiri wa baadhi ya
masharti ya kujiunga kama yana ishara
mbaya, aliongeza ;
“Siyo kila kitu mtu ajue , lazima yawepo
baadhi ya mambo mnayojua wenyewe tu ,
angalia hata shoo ya Diamond , ameweka
kiingilio kikubwa kwa sababu siyo kila mtu
lazima aingie , wengine wa oyaoya waishie
hukuhuku, huko kuna wenyewe , binafsi
nitafurahi sana nikipata chansi , hao waliomo
humo mbona hatuoni watoto wao wamekufa
au wazazi wao ? , ” alisema kwa kuhoji Baby .
 
kila mtanzania aliyetimamu lazma atakubali uwezo wa zito haijalishi umri,kabila,jinsi,wala dini ztto ni kipenzi cha watu,kasoro mataahira ambayo kuyatambua wala hutumii nguvu utaona cmmnt zao.
 
Huyu kichaa nae anatafuta kick tu.Ila sitoshangaa huenda akapata 1 night stand maana huyu baby madaha hana tofauti sana na diva.
 
Back
Top Bottom