Sio wote
Mi wakati niko bachela demu wangu akinitumia "baby nikwambie kitu" mara nyingi zilikua habari njema sana kwangu': Nimetoka home nakuja kwako muda huu--- msela najiona life nimelipatia[emoji23]
Baby boom limetoka ntakupitia tupange bajeti zetu[emoji23] [emoji23] enzi za chuo wallah ukimpata mwanamke anayekupenda hutachukia mapenzi.
Baby ile issue niliyokwambia Mzee kakubali amesema field nijaze mkoa uleee(mkoa ambao namimi nimejaza[emoji23] mbuzi kafia kwa muuza supu)
Baby nikwambie kitu...
Nisamehe kwa nilivyokukwaza jana ... I like that[emoji23] [emoji23]
Sasa mwenzangu wewe ukiona message ya hivo unajua mzinga[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Mwanamke ukimjenga vizuri pesa yako itakua yake na pesa yake itakua yako tena iko siku utakua umekwama unashangaa unatumiwa ela na demu wako kama surprise.. Haraka haraka unapiga simu kulikoni baby mbona umenitumia pesa umetoa wapi.... Boom limetoka... Mshahara umetoka najua huna ela kwa sasa baby tumia hiyo itakusogeza nikija home tutaongea[emoji23]
Mwanamke kama maji hana umbo maalumu(tabia), Maji hayana umbo maalumu ukiyaweka kwenye kibuyu yanachukua umbo la kibuyu, ukiyaweka kwenye ndoo yanachukua umbo la ndoo.
Ukiona demu wako anataka kukukomoa kila siku mizinga ujue kuna sehemu hujampatia ama wewe ni kicheche au demu huyo hakufai[emoji23]